Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeagizwa kutumia fedha kutoka vifungu ambavyo havina shida ya mifumo ili kutekeleza miradi mbalimbali ikiwepo ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya Msingi Makongolosi na vyumba vitatu vya Madarasa shule ya msingi Chunya mjini ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kusomea ili fedha husika zitakapopatikana zinarejeshwa eneo lake
Akizungumza jana tarehe 4/2/2024 Viwanja vya shule ya msingi Bwawani katika Maadhimisho ya kutimiza miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi kwa niaba ya chama mkoa wa Mbeya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya Ngugu Ndele Mwaselela amesema ni kazi ya chama kusikiliza kero za wananchi
“Mkurugenzi tumie fedha kutoka vifungu ambavyo havina changamoto kuanza kutekeleza ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule hii ya Makongolosi na ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Chunya Mjini, viongozi wa kamati za ujenzi fikeni ofisi ya Mkurugenzi jumatatu ili muanze kufuatilia vifaa na taratibu nyingine na madarasa yaanze kujengwa” Alisema Mwaselela
Mwaselela amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Elimu, sekta ya Afya ,Barabara na miradi mingine ambayo iimetekelezwa na inaendelea kutekelezwa Wilayani chunya na Tanzania kwa ujumla.
‘’Naomba niwape salamu za Mhe Rais ameleta hapa Chunya miradi mikubwa sana ya Elimu na tumetembelea na kuona Shule ya Msingi Amani imejengwa kama Chuo kikuu leo watoto wetu wanakwenda shuleni wanasoma na kukaa katika mazingira safi na salama, Pia vituo vya afya na taa za barabarani tunaona leo miaka 47 ya CCM tunaona mafanikio makubwa”. Alisema mhe, Mwaselela
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu John Maholani amekiri kuyapokea maagizo yote yaliyotolewa na kuahidi kuyatekeleza kwa kuyatafutia ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kupeleka lori la kubebe taka katika mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi pamoja na kero zingine.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Noel chiwanga amesema kuwa chama cha Mapinduzi ndicho kilichopewa jukumu la kusikiliza na kutatua kero za wananchi hivyo wao kama viongozi wako tayari kupokea maelekezo yote kutoka kwa mgeni rasmi lakini pia kusikiliza na kuzitolea majibu kero mbalimbali za Wananchi.
“Chama cha Mapinduzi ndicho chenye Jukum la kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi yawezekana huduma zinazotolewa zina weza kuwa na malalamiko sasi sisi ndio wenye Nyumba lazima tusikilize kero zenu na na tuone namna ya kuzitatu”. alisema Chiwanga
Aidha Mhe. Sailon Mbalawata wa kata ya Bwawani na Mhe,Kasimu Haule wameeleza mafaanikio Makubwa na miradi na mbalimali iliyotekelezwa katika kata hizo Ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za kisasa , kituo cha Afya , miundombinu ya Barabara na miradi mingine ambayo imetatuliwaa na kupuza kero mbalimbali za waanchi ikiwa ni pamoja na kupunguza msingamano wa wanafunzi darasani pamoja na kuboresha huduma za Afya.
Salvatory Mwandambile , Tumaini Mwamakula, Ibrahim Semsokwe na wengine wemeeleza changamoto mbalimbali ikiwemo kero ya Barabara ,uchakavu wa miundombinu soko la Makonolosi, Uhaba wa maji wakati wa kiangazi na umeme ambapo kero hizo zimeweza kupewa ufumbuzi na majibu papo hapokupitia Wataalam wa Halmashauri ya WIlaya ya Chunya pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi.
Maadhimisho yaho yameudhuriwa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika Ngazi mbalimbali , Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Wananchi Maadhimisho hayo yameenda sambamba na Kutembelea na kukagua miradi mbalimnali ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa ofisi ya Chama hicho , shule ya Msingi Amani na Kituo cha Afya cha Makongolosi.
Ndele Mwaselela akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Wananchi wakati alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Makongolosiyaliko fanyikia Maadhimisho ya miaka 47 ya CCM .
Afisa tarafa wa tarafa ya Kiwanja Ndugu Erick Nyoni akimwakilisha Mkuu wa WIlaya ya Chunyu akitoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Miradi mikubwa ya Maendeleo ilitokelezwa Wilayani Chunya.
Mhe. kassim Haule diwani wa kata ya Makongolosi akitoa mufafanuzi juu ya kero ya barabara ya Mwaoga katika Mkutano wa kusikiliza kero wakati wa maadhimisho ya ya sherehe ya miaka 47 ya chama cha Mapinduzi
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dr Andrew Darison akitoa maelezo kuhusu ukamilishwaji wa kituo cha Afya Makongolosi kwa Mgeni rasmi ndugu Ndele Mwaselela wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi alipotembelea na kukagua kituo hicho.
Salvatory Mwandambile katibu wa chama cha waendesha Boda boda Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi akitoa kero zinazowakabili kwa Mgeni rasmi ndugu Ndele Mwaselela wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.