Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga amewataka walengwa wote wa TASAF kuhakikisha wanapokea malipo ya Fedha kupitia kwenye akaunti zao za Benki au mitandao ya simu kwa Mujibu wa maelekezo wanayopatiwa na wawezeshaji wa TASAF ili kuhakikisha usalama wa fedha hizo unazingatiwa ndipo tuendelee kufanya vizuri katika kuzisimamia fedha hizo kama Serikali ya awamu ya Sita inavyoelekeza.
Ametoa kauli hiyo jana tarehe 16/05/2024 katika viwanja vya ofisi ya kata ya Matwiga iliyopo kwenye kijiji cha Isangawana, wakati akizungumza na walengwa wa TASAF kutoka kijiji cha Isangawana ikiwa ni sehemu ya kuhimiza matumizi sahihi ya fedha hizo kwa walengwa.
“Wale ambao hawajaanza kupokea fedha zao kupitia kwenye akaunti au mitandao ya simu, niwaombe tuanze kuchukua fedha wote kupitia kwenye akaunti au mitandao ya simu, asiwepo mtu yeyote anayepokea fedha mkononi mimi kama Mkuu wa wilaya naagiza kupitia kikao hiki asipewe, maana kuweka fedha kwenye akaunti au kwenye simu ndio utaratibu mzuri wa kulinda fedha zenu maana fedha hazitapotea na wala hazitaibiwa” Alisema Mhe Batenga
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za TASAF wilaya ya Chunya Mratibu wa TASAF wilaya ya Chunya Ndugu David Ngowo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuipatia fedhe zaidi ya Bilioni 1.7 (1,701,577,599.00/=) kwaajili ya kuwasaidia walengwa wa TASAF jambo linaloendelea kuimarisha ustawi wa wa wananchi wa wilaya ya Chunya kwa Ujumla wake.
“Fedha za TASAF wilaya ya Chunya zimetolewa katika awamu kumi na saba (17) kwa kipindi cha kuanzia Julai, 2023 mpaka May 2024. Huku Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikipokea Fedha kiasi cha shilingi Bilioni moja, milioni mia saba na moja, laki tano na sabini na sana mia tano tisini na tisa. Kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha hizo” Alisema Ngowo
Kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo ndugu Cutherth Mwinuka amemwambia Mkuu wa wilaya ya Chunya kwamba Halmashauri ya wilaya ya Chunya Inashika nafasi ya Tatu Kitaifa kwa matumizi ya mifumo ya Kibenki katika utekelezaji wa Shughuli za TASAF hivyo fedha za TASAF ziko salama kwa kiwango kikubwa
“Kwa wilaya ya Chunya asilimia tisini na nane ya wanufaika (98%) wanatumia mfumo wa kielektroniki kupokea malipo, Hivyo katika Taifa hili la Tanzania wilaya ya Chunya ni ya tatu kwa walengwa wa TASAF kupokea fedha zao kupitia simu na mitandao ya Kifedha”
Pamoja na Shughuli nyingene zilizofanyika kwenye Mkutano huo, Mkuu wa wilaya ya Chunya alikagua kaya za walenga wawili kwa niaba ya walengwa wengine wa TASAF ili kuona na kujiridhisha juu ya maelekezo, mafunzo na miongozo ya matumizi ya Fedha za TASAF kwa walengwa
Katibu Tawala wa wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero akizungumza kwenye Mkutano wa Mkuu wa wilaya na walengwa wa TASAF Isangawana
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Cuthbeth Mwinuka akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkuu wa wilaya na Walengwa wa TASAF uliofanyika Jana katika Kijiji cha Isangawana
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu David Ngowo akizungumza Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya pamoja na walengwa wa TASAF Jana kwenye Mkutano na walengwa wa TASAF
Diwani wa Kata ya Matwiga Mhe Mh. Frank E. Malambughi akiwasalimia walengwa wa TASAF kutoka Kijiji cha Isangawana wakati Mkuu wa wilaya ya Chunya alipowatembea na kuzungumza nao
Mkuu wa wilaya ya Chunya (Kushoto aliyenyoosha mikono akizungumza) akizungumzana na Bi Happy Mbaruk mnufaika wa TASAF kutoka Kijiji cha Isangawana alipokuwa anawatembelea wanufaika hao Nyumbani kwao
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.