• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

Aliyembaka mtoto wa dada yake afungwa maisha

Imewekwa: July 23rd, 2022

Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha Change Mohammed Mawanga(32) mkazi wa Mlimanjiwa Kata ya Mbugani kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka minne na kumsababishia maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Akisoma makosa ya mtuhumiwa katika kesi ya jinai namba 64/2022 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya James Mhanuzi,Mwendesha mashitaka wa Polisi Mazoya Luchagula ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa ametenda makosa hayo kwa nyakati tofauti mwezi aprili 2022 ambapo alikamatwa mei 5,2022.

Mazoya amesema makosa hayo ni kinyume cha sheria namba 130(1)(2) na 131(1)sura ya 16 ya makosa ya jinai iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 ambapo mshitakiwa alikana makosa yote.

Upande wa mashitaka umeleta mashahidi mbalimbali akiwemo mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambapo alimtamtambua mahakamani kama anko,mama wa mtoto,askari,afisa ustawi wa jamii na daktari aliyewasilisha PF 3 iliyoambatana na vipimo vilivyoonesha mtoto kubakwa na kuingiliwa kinyume cha maumbile.

Baada ya Hakimu James Mhanuzi kusikiliza upande wa mashitaka na mshitakiwa mahakama iliridhika pasipo shaka na upande wa mashitaka pia kubaini kuwa mshitakiwa anayo kesi ya kujibu.

Akijitetea Change Mohammed Mawanga amesema kuwa hakutenda makosa hayo na kwamba anasingiziwa tu na katika maombolezo yake aliiomba mahakama kumwachia huru kwa kuwa ana wategemezi akiwemo mama yake,mke na wadogo zake wanaomtegemea.

Kwa upande wa mashitaka Mazoya Luchagula alisema mbali ya mshitakiwa kutokuwa na matukio mengine ya uhalifu ameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa hasa ikizingatiwa mtoto aliyefanyiwa ukatili ana umri wa miaka minne tu isitoshe ni mtoto wa dada yake.

Aidha Hakimu James Mhanuzi baada ya kusikiliza pande zote mahakama imemtia hatiani kwa makosa yote mawili ambapo kosa la kumbaka mtoto chini ya miaka 18 kifungu cha sheria 154(1)(2) sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022 adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Kosa la pili la kumlawiti mtoto chini ya miaka 18 adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Mhanuzi amesema adhabu hiyo iwe fundisho kwa mshitakiwa na wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo hasa kutokana na kukuthiri vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto Wilayani Chunya vitendo vinavyohusishwa na imani za kishirikina kwa madai ya kupata dhahabu pindi wanapojamiana au kuwalawiti watoto wadogo.

Hivyo kwa makosa yote mshitakiwa atatumikia adhabu zote mbili kwa pamoja na maisha yake yote kuishia gerezani.

Nje ya mahakama Afisa Ustawi wa Jamii Nashitabo Mwalende alisema mahakama imetenda haki kwani kumekuwa na vitendo vingi vya ukatili dhidi ya watoto.

Mahakama hiyo bado inaendelea kusikiliza kesi za ubakaji na ulawiti ikiwemo ya baba kumbaka mwanawe hukumu itakayotolewa mwezi agosti mwaka huu.

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • TARAFA YA KIPEMBAWE CHUNYA YAJIDHATITI KUWATUMIKIA WANANCHI.

    March 21, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.