Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwalimu Kiduma Mageni amewafunda walimu wa Shule za Msingi na awali wilayani Chunya kwakuwambia lazima wayapende mazingira yao ya kazi kwani muda mwingi wa Maisha yao hutumia kuwepo mazingira ya Shule na kwakuyapenda Mazingira hayo itavutia walimu kufundisha lakini itavutia wanafunzi kusoma kwa bidii
Ametoa maelekezo hayo mapema leo tarehe 13/05/2024 wakati akizungumza na walimu wakuu, walimu wakuu wasiaidizi ,Maafisa elimu Kata pamoja na walimu wa taaluma kwenye kikao kilichoketi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) kikoa chenye lengo la kuendelea kuimarisha ufundishaji wa wanafunzi ili kufikia lengo la kufanya vizuri kwenye mitihani ya ndani na ya nje
“Hakikisheni pale shuleni ni sehemu ya kuishi hivyo mazingira yawe yenye kuvutia na pia ongezeni ubunifu katika kufanya mazingira ya Shuleni yanakuwa yenye kuvutia lakini ubinifu katika ufundishaji wa Masomo ili kuhakikisha wanafunzi katika Shule zenu wanafanya vizuri”amesema Mageni
Mwalimu Mageni pia amewataka uongozi wa Shule kwa maana ya Mkuu wa Shule, Mwalimu Mkuu msaidizi pamoja na Mtaaluma kuhakikisha wanawajali walimu na watumishi wengine waliopo katika shule zao, kwakufanya hivyo kila mmoja atajituma katika kutekekeleza majukumu yake jambo litakalosaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wao.
“Wakuu wa Shule na viongozi wa Shule kwa Ujumla hakikisheni mnawajali walimu na watumishi wengine wanaofanyakazi chini yenu, Kwa kufanya hivyo mtawafanya wajitume katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku jambo litakalopelekea ufaulu stahiki katika shule husika, hivyo wakati mwingine kufeli ni kuamua tu”amesema Mageni
Aidha Mwalimu Mageni ameongeza kuwa kila Shule kupata ufaulu asilimia mia inawezekana endapo kila mwalimu atasimama katika nafasi yake na kujituma ikiwa ni pamoja na walimu wakuu kuwajua walimu wao na masomo yao wanayofundisha lakini pia kujiwekea malengo na kuhakikisha yanatimia .
Naye Afisa elimu awali na msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu Ferd Y. Mhanze ametoa rai kwa Walimu kuhakikisha maelekezo yote na maagizo kutoka kwa Afisa elimu wa Mkoa wanakwenda kuyafanyia kazi kwaajili ya kuhakikisha Chunya inafanya vizuri katika taaluma
Kikao cha Afisa elimu Mkoa wa Mbeya kimehusisha Maafisa elimu Msingi kutoka Wilayani, Maafisa elimu kata, Walimu wakuu, Walimu wakuu wasaidizi,Walimu wa Taaluma, Mdhibiti ubora, na afisa TSC lengo likiwa ni kujadili mambo mbalimbali katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inafanya vizuri katika taaluma kwani Chunya Bila Kufeli Inawezekana.
Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwalimu Kiduma Mageni akizungumza na walimu wakati wa kikao chake kilichoketi leo tarehe 13/05/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Afisa Elimu awali na Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalim Ferd Y Mhanze akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Afisa Elimu Mkoa na walimu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Walimu wa Shule za awali na Msingi wakiendelea kufuatilia Kikao na aliyesimama Mbele akizungumza ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Mwalimu Kiduma
Chunya bila kufeli inawezekana, Walimu, viongozi na wananchi tushirikiane kuhakikisha watoto wetu wanafanya vizuri
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.