1.0 UTANGULIZI
Asilimia 87 ya wakazi wa wilaya ya Chunya wanategemea kilimo na kilimo ndiyo huchangia kwa kiwango kikubwa sana uchumi wa Wilaya.
Wilaya inakadiriwa kuwa najumla ya eneo lenye ukubwa wa hekta 1,315,000 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo linakadiriwa kuwa ni hekta 1,035,400 na jumla ya hekta 79,072 ndizo zilizotumika kwa kilimo cha mazao ya chakula, biashara na bustani(mboga na matunda) katika msimu wa kilimo 2016/2017.
Hata hivyo eneo linalolimwa hubadilika kila msimu kulingana na malengo ya wakulima na mwelekeo wa hali ya hewa
Mazao ya chakula yanayolimwa ni Mahindi, Viazi vitamu, Maharage, Ulezi, Mtama, Mpunga, Muhogo na Kunde. Mazao ya biashara ni Tumbaku, Karanga, Alizeti, Ufuta na Choroko.
Wilaya ina wastani wa joto kati ya nyuzi za sentigredi 21 na 23. Wilaya hii hupata aina moja ya mvua (Unimodal rainfall pattern) yenye wastani kati ya milimita 500 na1000 kwa mwaka. Msimu wa mvua huanzia mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi Aprili na kipindi chenye mvua nyingi ni kati ya mwezi Januari na Machi.
3.0 KANDA ZA MAZAO (AGRO – ECOLOGICAL ZONES)
Wilaya ina kanda kuu 2 nazo ni ukanda wa madini na ukanda wa miombo.
3.1 Ukanda wa madini : Ukanda huu unajumuisha maeneo yote ya Tarafa ya Kiwanja yenye kata 11, vijiji 19 na mitaa 35. Mazao yanayolimwa ni Mahindi, Maharage, Mtama, Karanga, Viazi vitamu, Ulezi, Mihogo na Alizeti
3.2 Ukanda wa miombo : Ukanda huu unajumuisha maeneo yote ya Tarafa ya Kipembawe yenye kata 9 na vijiji 24. Mazao yanayolimwa ni Mahindi, Tumbaku, Alizeti, Kunde, Choroko, Maharage, Mihogo, Viazi vitamu, Ulezi na Karanga
KUSOMA ZAIDI BONYEZA HAPA: SEKTA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA.pdf
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.