Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwl. Farida Mwasumilwe ametoa nasaa mbalimbali kwa walimu wa Shule za Msingi ili kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ikiwa ni pamoja na taratibu za usajili wa wanafunzi, uzaji wa taarifa mbalimbali kwenye mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni, utawala bora, uwajibikaji , usimamizi wa rasilimali na miradi ya shule pamoja na mambo mengine mengi.
Nasaa hizo amezitoa leo tarahe 16/01/2026 wakati wa kikao cha tathimini na kuweka malengo au matarajio ya taaluma kwa mwaka 2026 na walimu wa taaluma, walimu wakuu na maafisa elimu shule za msingi kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Niwaombe tuzingatie muda wa usajili kulingana na taratibu za baraza la mitihani, lakini pia kwa shule binafsi kulipa malipo ya mitihani ya watahiniwa kwa wakati , lakini suala jingine niombe tutumie kikamilifu mfumo wa ujazaji taarifa Shuleni (SIS) ikiwa ni pamoja na masuala ya likizo,maudhurio ya wanafunzi na mambo mengine mbalimbali”.amesema Mwl Farida.
Aidha, Mwl Farida ameendelea kuwakumbusha Shule binafsi kuhakikisha zinaendelea kuzingatia taratibu na miongozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikataba ya ajira kwa watumishi wao na kuwachangia katika mifuko mbalimbali, kuzingatia taratibu za usajili wa wanafunzi hususani wanaohamia na mambo mengine mengi.
Vilevile, Mwl Farida amesisitiza suala la utawala bora ikiwa ni pamoja na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu mbalimbali, kuwa wazi katika taarifa za fedha ,kuzingatia taratibu na miongozo mbalimbali ya shule pamoja na uzimamizi bora wa rasilimali za Shule ikiwemo thamani mbalimbali za Shule na miundombini.
Wakizungumza kwa niaba ya walimu wengine walioshiriki kikao hicho Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kiwanja, Mwl. Hadija Issa amesema wamejipanga kuhakikisha Wilaya ya Chunya inaongoza kwenye ufaulu wa matokeo ya darasa la nne na darasa la saba kwa mkoa wa Mbeya.
“Tumejipanga kimatokeo kuongeza ufaulu zaidi, kwa changamoto zilizojitokeza kwenye matokeo ya mwaka 2025 tunazifanyia kazi na kuongeza ufaulu kwa mwaka huu 2026, tunataka kuwa namba moja kwa mkoa wa Mbeya kwenye matokeo ya darasa la nne na darasa la saba” amesema Mwl. Hadija.
Kwa upande wake Mwalimu Frank Sanga wa Shule ya Msingi Mapongolo, amesema, sasa ni wakati wa kuyafanyia kazi mapungufu yote tuliyoyabaini kwenye tathmini ya kikao hicho ambapo kwa mwaka huu 2026 hawatarudi nyuma tena, wamejipanga kupandisha kiwango cha taaluma kwa shule za msingi Wilaya ya Chunya.
Kikao hicho mbali na kutoa nasaha pia kimesikiliza kero mbalimbali za walimu, changamoto, na kuangazia njia za utatuzi wa changamoto hizo kwa lengo la la kuboresha ili kujipanga kufanya vizuri kitaaluma na kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuwa mfano wa kuigwa kitaaluma na Halmashauri nyengine Mkoa wa Mbeya.

Washiriki wa kikao cha tathmini na malengo ya taaluma kwa mwaka 2026 Wilaya ya Chunya wakifuatilia kwa makini hotuba ya Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Mwl. Farida Mwasumilwe. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sapanjo leo tarehe Januari 16, 2026.

Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwl. Farida Mwasumilwe akitoa hotuba yake kwa washiriki wa kikao cha tathmini na malengo ya taaluma kwa mwaka 2026 Wilaya ya Chunya. Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sapanjo leo tarehe Januari 16, 2026.

Washiriki wa kikao cha tathmini na malengo ya taaluma kwa mwaka 2026 Wilaya ya Chunya wakifuatilia kwa makini hotuba ya Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Mwl. Farida Mwasumilwe. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sapanjo leo tarehe Januari 16, 2026.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.