• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI TAREHE 12 – 16 MACHI, 2018 UKUMBI WA AICC, ARUSHA

Imewekwa: March 21st, 2018

        

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MH. MRISHO GAMBO AKIONGEA NA MAAFISA HABARI, MAWASILANO SERIKALINI



kuanzia tarehe 12-16 Machi kilifanyika kikao kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini. ambapo Hotuba, Mada na Mijadala Pamoja na Maazimio Mbalimbali Viliwasilishwa.

 ifuatayo ni hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Akimkaribisha Mgeni Rasmi wa Kikao hicho Mh. Waziri wa Habari, Ndg. Harisson Mwakyembe; HOTUBA YA KATIBU MKUU.pdf


UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI KILICHOFANYIKA UKUMBI WA HAZINA NDOGO MJINI DODOMA MACHI 13-17, 2017.

1. Kuanzishwa mfumo wa kuweka malengo na upimaji wa Taasisi katika eneo la mawasiliano.

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo iliandika barua yenye Kumb NA FA/238/292/01B/21 ya tarehe 27 Machi, 2017 na

kutumwa kwa Wizara zote, Wakala na Idara zinazojitegemea pamoja na Taasisi zote za Serikali.

Barua hiyo ilieleza umuhimu wa taasisi kutekeleza malengo ya kitaifa ya Mawasiliano pamoja na Maazimio mengine ya Kikao

kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini cha mwaka 2017.  

Aidha, kufuatia barua hiyo, Ofisi ya Rais TAMISEMI iliandika barua yenye Kumb Na AB.156/174/01 ya tarehe 9, Mei, 2017

kwenda kwenye Mikoa na Halmashuri zote nchini ikiambatanishwa na malengo ya Kitaifa ya mawasiliano yaliyopitishwa wakati

wa kikao kazi pamoja na maazimio kwa utekelezaji.

  Wizara zote zilipewa taarifa kuwa utekelezaji wa Malengo utaanza kupimwa rasmi kuanzia Julai 2017.

Baadhi ya Wizara zimekuwa zikiwasilisha taarifa hizo Idara ya Habari – MAELEZO kila mwezi ambapo pia kumekuwa na Mikutano

kati ya Msemaji wa Serikali na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara. Taarifa zinaonyesha bado utekelezaji

wa Malengo ya Kitaifa ya Mawasiliano sio mzuri.

Hatujapata taarifa za utekelezaji kutoka kwa Maafisa Mawasiliano wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi

nyingine za Serikali.

Tathmini ya Wizara zilizotekeleza malengo ya Kitaifa na kuwasilisha taarifa zao inaonyesha waliofanya vizuri na wale ambao

hawajawasilisha taarifa zao.


2.Maafisa Habari/Mawasiliano kutekeleza Sheria ya Huduma ya Habari na Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa na Kanuni zake kwa

kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara na kwa wakati.


    Idara ya Habari MAELEZO imekuwa ikifanya mikutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kitaifa,

Msemaji Mkuu wa Serikali amekuwa akishirikisha Wizara na Taasisi husika kupata taarifa na takwimu katika masuala husika.

Taarifa hizo zimekuwa zikitangazwa kupitia Radio, Televisheni, Magazeti na Mitandao ya Kijamii ikiwemo Blogs, Maelezo TV,

Facebook, Twitter ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Makundi mbali mbali ya Instagram.

Aidha, Ofisi ya Rais TAMISEMI iliandika barua yenye kumb. Na. EB.151/297/104 ya tarehe 06 April, 2017 kuwataka Wakuu wa

Mikoa kuhakikisha kuwa Tovuti zote za Mikoa na Halmashauri zinakuwa na taarifa za kutosha zinazotolewa kwa wakati.

Barua hiyo imeelekeza mikoa kuhakikisha kuwa Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri wanashirikishwa katika shughuli zote

za mikoa na halmashauri kwa kuingia katika vikao vyote muhimu ili kuwa na uelewa mpana wa shughuli za mkoa au halmashauri

husika na kutoa ushauri utakaofanikisha ofisi hizo kutoa mawasilia kwa umma kwa ufanisi.

Tathmini fupi tuliyoifanya inaonyesha Wizara, Mikoa na Halmashauri nyingi zinafanya vizuri kwenye eneo la kuweka taarifa

kwa wakati kwenye tovuti.

Hata hivyo, bado kuna changamoto kwa baadhi ya taasisi katika kuweka taarifa kwa wakati kwenye Tovuti zao.


3. Maelekezo yatolewe kwa taasisi zote kutenga bajeti na kununua vitendea kazi  kwa ofisi za Mawasiliano.


   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI walitoa maelekezo mahususi kuhusu

suala la Taasisi kutenga bajeti za kununulia vitendea kazi  kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini. Maelekezo hayowakati wa

uzinduzi wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri mjini Dodoma  mwezi machi 2017 mara baada ya Kikao Kazi. Maelekezo hayo

yalisisitizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI   katika barua yake yenye Kumb. Na. EB.151/297/104 ya tarehe 06

April, 2017.


Aidha, aliyekuwa Waziri wa Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo katika kipindi  2016/2017 akiwa katika ziara zake Mikoani

alisisitiza kila Mkoa na Halmashuri kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kuwanunulia vifaa Maafisa Habari na Mawasiliano

Serikalini.

Bado kuna changamoto ya baadhi ya ofisi kutokuwa na vitendea kazi pamoja na watendaji wa ofisi za Mawasiliano kutoruhusiwa

kuingia kwenye vikao vya maamuzi. Wapo waliojitokeza kueleza hali halisi.


4. Mikoa iandae ratiba za mikutano na vyombo vya Habari kwa Halmashauri, Manispaa , Majiji, Miji na Taasisi zilizoko

katika mkoa husika.


      Wizara ya Habari iliandika barua yenye Kumb NA FA/238/292/01B/21 ya tarehe 27 Machi, 2017 na kutumwa Ofisi ya Rais

TAMISEMI. Barua hiyo ilieleza kuhusu umuhimu wa mikoa kutekeleza maazimio ya Kikao kazi cha mwaka 2017 likiwemo suala la  

kuitaka Mikoa kuandaa na kutekeleza ratiba ya mikutano na Vyombo vya Habari.Hatuna taarifa za utekelezaji wa azimio hili.


5.  Maafisa Habari wa Taasisi, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa waruhusiwe kuingia vikao vya maamuzi


    Wizara ya Habari iliandika barua yenye Kumb Na. FA/238/292/01B/21. Kufuatia barua hii Ofisi ya Rais TAMISEMI

waliandika barua yenye Kumb. Na. EB 151/297/01/104 ya tarehe 06 April 2017 kwenda kwa Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara

ili Maafisa Mawasiliano wa Sekretariet za Mikoa na Serikali za Mitaa wapatiwe Vitendea kazi vikiwemo Kamera, Kompyuta

mpakato, Inteneti na pia waruhusiwe kuingia kwenye vikao vya menejimenti.

Baadhi ya Maafisa Habari wa Mikoa wanaingia kwenye vikao vya Menejimenti. Mikoa  iliyothibitisha kuwa Maafisa Habari wake

wanahudhuria vikao vya Menejimenti ni Simiyu, Pwani, Arusha, Shinyanga, Lindi, Dodoma, Songwe na Kigoma.

Bado kuna  changamoto ya baadhi ya Maafisa Habari wa Sekretarieti za Mikoa  na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoruhusiwa

kuingia kwenye vikao  vya Menejimenti.


                                                                            

Waziri Wa OR-TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo(wa pili kulia) akiwa na katibu mkuu wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi(mwenye koti la Pinki), na Msemaji wa Serikali Ndg. Hussein Abas

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.