• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

WATUMISHI WATAKIWA KUENDELEA KUSIMAMIA MAADILI NA WAJIBU WAO.

Imewekwa: February 3rd, 2025

Hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya Wilaya  Mhe.James Mhanusi amewataka  watumishi wa kada zote kuendelea kusimamia maadili na  kutekeleza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi  na  kujiepusha na vitendo visivyo vya kimaadili  huku wakizingatia misingi ya kutenda haki wawapo kazini  ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma za utoaji haki kwa wananchi zinapatikana kwa wakati.

Hayo ameyasema leo tarehe 3/2/2025 wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki  ya sheria nchini  yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo) yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya 2050: nafasi ya taasisi zinazosimania haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo,”

“Mahakama ya Wilaya ya Chunya  tumeendelea kukemea vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kwa watumishi  na kukumbushana kuhusu maadili na wajibu wetu tuwapo kazini,lakini pia kuhakikisha huduma za utoaji haki kwa wananchi zinapatikana kwa wakati  na kuendelea kusirikiana vema na wadau wote na wananchi kwa ujumla  ili kutimiza wajibu huo”. Alisema Mhe. Mhanusi

Vile vile Mhe. Mhanusi amesema kuwa Mahakama imeendelea kusikiliza mashauli mbalimbali  na kutoa nakala za hukumu  kwa wakati , kusikiliza malalamiko ya wadau na kuyatolea majibu  kwa wakati hali inayofanya wananchi  kupata haki zao kwa wakati lakini pia inasaidia  mahakama kutokuwa na mulundikano wa mashitaka.

 Katibu tawala wa  Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya   amewataka wadau wa mahakama kuendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao na kutenda haki ili kupunguza mrundikano wa majukumu upande mmoja kwani kila  taasisi inayosimamia haki  ikitekeleza majukumu yake  itasaidia kupunguza  mzigo wa majukum  katika taasisi nyingine .

Naye Mkuu wa Mashitaka Wilaya ya Chunya  ndugu Mwajabu Tengeneza amesema kuwa  madhumni ya siku ya sheria ni pamoja na kutathimini dhana ya utoaji wa haki  na mchango wa kila taasisi inayotoa haki, kutoa elimu juu ya haki kwa jamii  na kuwaombea majaji na mahakimu  ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kutenda haki kwa hekima na busara.

Wadau mbalimbali  ikiwa ni  pamoja na Ustawi wa Jamii , jeshi la polisi , takukuru na wadau wengine  wameeleza umuhim wa  wiki ya sheria kwani imekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali yahusuyo sheria  na kuwawezesha wananchi kutambua wajibu na haki zao katika jamii na taifa kwa ujumla.

 Kilele cha maadhimisho ya wiki  ya sheria nchini  huadhimishwa kila mwaka mwanzoni mwa mwezi February ambapo kwa mwaka huu  maadhimisho yalitanguliwa na wiki ya sheria iliyoanza tarehe 25/1/2025 katika Wilaya ya Chunya ,uzinduzi wa wiki ya sheria ulifanyika katika kijiji cha Kambikatoko kata ya Kambikatoto na kilele cha maadhimisho kimefanyika leo tarehe 3/2/2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri (Sapanjo) uliopo kata ya Itewe  na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, vyama vya siasa wadau wa Mahakama  , kwaya  kutoka madhebebu mbalimbali na  wanafunzi .

Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya Katibu tawala wa Wilaya ndugu Anakleth Michombero amewataka wadau kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu , hayo ameyasema wakati wa kilile cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo).

Shekh Kasimu Issa akiomba dua wakati  wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo).

Watumishi wa Mahakama wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu wakati wa kilile cha maadhimisho ya wiki ya sheria Wilayani Chunya.

Viongozi wa Madhehebu mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu wakati wa kiklele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo)

 

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.