• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

WATENDAJI TUMIENI VIZURI MAHUDHURIO NA MAJINA YA WATU.

Imewekwa: April 4th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu mwandamizi wa Uhamiaji Mhe.Mbarak Alhaji Batenga  amewataka watendaji wa vijiji kutumia vizuri majina na mahudhurio ya watu  wakati wakuaandaa mhitasari mara  baabda ya mkutano kufanyika  kwa kuhakikisha wanaandika yale yaliyojadiliwa na wajumbe  kwenye Mkutano na sio mambo mengine .

Hayo ameyasema April 3, 2024 wakati wa kikao kilichoketi katika kanisa la Pentekoste kijiji cha Ifumbo kata ya Ifumbo cha kusuluhisha mgogoro baina ya familia  ya Wayanga  waliokuwa wa miliki wa eneo kabla ya kununuliwa na mwekezaji pamoja na   wawekezaji wa eneo hilo.

“Kwenye  vijiji kumekuwa na tabia moja mnapoitisha Mkutano  watu wakaandika mahudhurio yao  na kusaini  inakuwa kama wamewapa kibali cha kwenda kufanya mnachotaka kufanya mnapokwenda kuandika mhitasari mwenyekiti na mtendaji mnaanza kuumba Mhitasari mwingine tofauti na yaliyojadiliwa kwenye mkutano hivyo achene kutumia majina na mahudhurio ya watu vibaya” alisema Mhe Batenga

Aidha amewaasa viongozi wa kijiji  cha Ifumbo  kutofautisha migogoro baina ya mtu mmoja na mwingine na migogoyo ya jamii na kijiji ili kuondoa taharuki katika jamii  kwani hali hiyo inaweza   kuzalisha migogoro mingine  hivyo mgogoro wa mtu mmoja na mwingine isihusishe na jamii nzima iliyopo katika kijiji.

Akiongea kwenye kikao hicho kwa niaba ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chunya, katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya ndugu Msafiri Mayeye, amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kazi nzuri anayoifaanya ya kushughulikia changamoto mbalimali za wananchi na kumuomba aendelee kuwafuatilia wawekezaji hao mpaka watakapofikia hitimisho la mgogoro wao kwani Chama cha mapinduzi  kinawakaribisha wawekezaji na hakitaki kuwapoteza wawekezaji hao

Naye Diwani wa kata ya Ifumbo Mhe.Weston Mpyila akatoa rai kwa watu wanaomiliki maeneo kuwa wakweli na wa wazi pindi wanapotaka kupangisha au kuuza maeneo yao ili kuzuia migogoro ambayo inaweza kujitokeza  huku akiwaomba wakwekezaji ndugu Lukasi Mwamenza na ndugu Aidani Msigwa kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao lakini pia familia ya Wayanga waliokuwa wamiliki wa awali kuwa wakweli na kuweka kila kitu wazi wanapotaka kufanya jambo .

“Nitoe rai kwa watu wengine wenye maeneo wanapotaka kuyauza au kuyapangisha kuweka kila kitu wazi, lakini pia niombe hawa wawekezaji wawili msigwa na Luka waone namna wakae na  kuumaliza mgogoo huu kwasababu wao ndio wenye kuumaliza ili wawe na Amani na mambo mengine yaweze kuendelea “alisema Mhe Mpyila

Kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa sita kwa lengo la kuumaliza mgogoro baina ya familia na wawekezaji kimehudhuriwa na kamati ya ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuanzia Ngazi ya wilaya , kata na tawi, watalamu mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Pamoja na Viongozi kutoka Taasisi  mbalimbali na viongozi wa kata na kijiji.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga akizungumza na wajumbe wa kikao  wakati wa  kusuluhisha mgogoro  wa ardhi baina ya familia iliyokuwa ikimiliki eneo lililo nunuliwa na mwekezaji  pamoja na wawekezaji hao  katika kijiji cha Ifumbo 

Katibu wa umoja wa Vijana kupitia  chama cha Mapinduzi ndugu Msafiri Mayeye akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Chunya  kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wakati wa kikao cha kusuluhisha mgogoro baina ya familia iliyokuwa ikimiliki eneo lenye mgogoro na wawekazaji kilichoketi katika kanisa la Pentekoste katika kijiji cha Ifumbo

Diwani wa kata ya Ifumbo Mhe Weston Mpyila akitoa rai kwa wananchi wa kijiji cha Ifumbo wanaomiliki maeneo kuwa wakweli na kuweka kila kitu wazi pale wanapotaka kuuza maeneo yao ili kuzuia migogoro inayoweza kujitokeza   kutokana na udanganyifu


Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.