• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

WATENDAJI KATA CHUNYA DC WAONGEZEWA UJUZI WA UKUSANYAJI WA MAPATO

Imewekwa: December 18th, 2023

Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya manispaa ya Ilemela  kwaajili ya kuongeza ujuzi na mbinu    katika ukusanyaji wa mapato  ikiwa ni jitihada za kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kukusanya mapato ya Halmashauri kwenye vyanzo mbalimbali vya Mapato.

Ziara hiyo ni kutokana na  Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu kambona  kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na watendaji  wa kata katika ukusanyaji wa mapato zimepelekea Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato katika mkoa wa Mbeya hivyo ameamua  kuwapa motisha watendaji  hao  ili kujifunza njia mbalimbali za ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya manispaa ya ilemela Mkoani Mwanza

Awali akielezea lengo la ziara hiyo Mkuu wa Msafara Afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Moses Ngole amesema kuwa ziara ya watendaji kata imelenga kujifunza  namna mbalimbali za ukusanyaji wa mapato  kutoka katika vyanzo mbalimbali ili sisi pia tukaendelee kuimarisha zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Afisa Biashara wa Halmashauri hiyo  Bi Elizabeth Swagi amefurarahishwa na ugeni wa watendaji kutoka Chunya na kusema kuwa  kuna vitu ambavyo watajifunza kutoka kwao ikiwa ni pamoja na njia mbalimbali zinazotumika kukusanya mapato zinazoongozwa na sheria ndogo ndogo za Halmashauri.

 Miongoni mwa njia za ukusanyaji wa mapoto walizojifunza watendaji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni pamoja na kutumia Mahakama inayotembea (Mobile court) ambapo njia hiyo imekuwa ikitumiwa na maafisa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pale ambapo wahusika wanashindwa kilipa mapato kwa utaratibu uliowekwa hivyo kufikishwa katika hatua za mahakama.  

Nae  Afisa mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ndugu Nicolaus Kawana  ameeleza vyanzo mbalimbali vya mapato na jinsi ambavyo wamekuwa wakikusanya mapato katika vyonzo hivyo  ikiwa ni pamoja na stendi ya mabasi, leseni za biashara , nyumba za kulala wageni na vyanzo vingine vingi ambavyo vimekuwa vikiingizia halmashauri hiyo mapato.

Wakiwawakilisha watendaji kata wenzao kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya  ndugu Ayubu  Masota, , Egitho Bilali, Monica Magasha  wameweza kuuliza maswali mbalimbali kwaajili ya kuongeza uelewa zaidi ikiwa ni pamoja na njia wanazotumia kukusanya ushuru wa taka,  ushuru wa mabasi na nyumba za kulala wageni na ni kwa namna gani njia ya Mahakama inayotembe imefanikiwa na changamoto zake.

Ziara ya watendaji wa kata imejumuisha Maafisa Utumishi, Afisa biashara, Afisa Tehama, Afisa mipango na Uratibu na Mhasibu, ziara hiyo imedumu kwa siku moja na  wameweza kutembelea baadhi ya vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na  Stendi kuu ya mabasi ya Nyamhongolo na Soko la samaki Mwaloni ambapo wamejifunza na kujionea vyanzo mbalimbali jinsi vinavyoiingizia mapato manispaa ya Ilemela

Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wakijiandaa kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela tayari kwa Mafunzo

Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na maafisa wengine kutoka Makao makuu ya wilaya wakipewa maelekezo na Bwana Wilhadius Buberwa Meneja Uvuvi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.