Idara ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Chunya yaendesha mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu mbalimbali katika vitengo na Idara za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuhusu uandaaji wa mpango wa bajeti katika mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa.
Akizungumza leo Septemba 30, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Chunya (Mwanginde Hall) muwezeshaji wa mafunzo hayo, ndugu Fredy Mwangalaba amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo Idara na vitengo kuandaa mpango wa bajeti katika mamlaka za serikali za mitaa.
“Mafunzo haya ya siku mbili ya uandaaji wa mpango wa bajeti yameanza leo Septemba 30, 2025 na yatahitimishwa kesho Oktoba 1, 2025 lengo ni kuwaongezewa uwezo wataalamu kuandaa mpango wa bajeti” amesema Mwangalaba.
Mafunzo ya mpango wa bajeti yamejuisha wataalamu wa Idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambapo mafunzo hayo yanatajwa kuongoza tija katika uandaaji wa mpango wa bajeti utakaowezesha kufikia malengo mbalimbali kwa ufanisi.
Muwezeshaji wa mafunzo, ndugu Fredy Mwangalaba akiendesha mafunzo ya Uandaaji wa Mpango wa Bajeti katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa
leo Septemba 30, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya(Mwanginde Hall).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mpango wa uandaaji wa bajeti wakisikiliza kwa makini mada iliyowasilishwa na muwezeshaji ndugu Fredy Mwangalaba
leo Septemba 30, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya(Mwanginde Hall)
Washiriki wakifuatilia kwa karibu mada zilizotolewa katika mafunzo ya siku mbili ya mpango wa uandaaji bajeti katika mamlaka za serikali za mitaa
katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya leo Septemba 30, 2025.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.