• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

WANANCHI KAMBIKATOTO WAISHUKURU SERIKALI KWAKUJENGA SHULE MPYA YA SEKONDARI

Imewekwa: October 9th, 2023

Wananchi wa kata ya Kambikatoto wilayani Chunya wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia fedha kiasi cha shilingi milioni 583,180,028 ili kujenga shule ya sekondari katika kata hiyo ambayo  pamoja na ukubwa wa kijiografia wa kata hiyo hata umbali kutoka kata hiyo mpaka kata nyingine ilikuwa bado haina shule ya sekondari ya kata.


Wakizungumza mbele ya kamati ya fedha, uongozi na mipango ya baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati kamati hiyo ilipopita kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wananchi wamesema serikali ina wajali sana kwani si muda mrefu kituo cha afya kambikatoto kimejengwa na sasa shule ya sekondari inajengwa.


“Tunashukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan kutujengea Shule ya Sekondari  yenye vyumba karibu kumi na mbili (12) kwenye Kata yetu jambo ambalo mimi sikuwahi kufikiria, Mimi nilijua tutaanza na madarasa mawili au matatu hivi, lakini serikali kwa wakati mmoja vyumba vya madarasa karibu 12 kwakweli tunaishukuru sana serikali. Alisema Ndugu Mwita Chacha.


“Mweshimiwa mwenyekiti wa Halmashauri sisi tunakushukuru wewe na kamati yako kuja kututembelea ili kukagua mradi huu lakini pia tunaishukuru sana serikali kutuletea mradi huu lakini pamoja na hayo tunaomba utusaidie kutazama upya bei za milango na fremu zake bei iliyowekwa ni sawa na bei za mjini wakati huku sisi bei za mbao zina nafuu kuliko mjini pia wananchi wengi huko mtaani wanamashaka na eneo hili eneo la bei za milango na fremu zake” Alisema Mathias Aloice Songo.


Naye Blandina Chingwile alisme “Mwenyekiti pamoja na kamati yako tunakushukuru kuja kutembelea mradi huu na kipekee sana tunaishukuru serikali kwa kutupatia mradi huu, Tulifanikiwa katika ujenzi wa kituo cha afya hatuwezi kushindwa kusimamia ujenzi wa shule hii hivyo mwenyekiti wewe uwe na amani kabisa. Pia usisite kuja au hata kupiga simu pale unaposikia changamoto maana lengo la serikali ni kutusaidia kutatua kero kwa wananchi wake”.


Kamati ya fedha, uongozi na Mipango (FUM) imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule hiyo kwani ni yao na itawasaidia wao wenyewe na familia zao na kwakufanya hivyo watakuwa wametekeleza na kuulinda utaifa na uzalendo wao kwani serikali inapowaletea fedha haina maana wananchi hawatakiwi kushiriki kabisa.


Aidha kamati hiyo kupitia mwenyeki wake Mhe Bosco S Mwanginde imewaagiza viongozi wanaosimamia mradi huo kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha inayotokana na nguvu za wananchi wa kata hiyo na baada ya kupata taarifa hiyo kamati hiyo itafanya ziara tena ili kuzungumza na wananchi maana serikali ya awamu ya sita inataka uwazi na ushirikshwaji wa jamii kuwa kipaumbele cha kwanza.


Kaimu afisa Elimu sekondari Mw. Nikusuma Kamoma amewataka wananchi kusimamia vizuri matumizi ya pesa hizo jambo ambalo kwanza litawapa sifa njema na nzuri lakini pia pesa zitakazo baki zinaweza kuanza mradi mwingine katika kata hiyo jambo ambalo litafanya kata hiyo kuwa na kasi katika maendeleo lakini kinyume chake mtaichafua wilaya ya Chunya jambo litakalosababisha wilaya ikakosa uaminifu na kupelekea serikali kusita kuleta pesa sababu tu usimamizi mbaya.


Kata ya Kambi katoto ina jumla ya wanafunzi 298 wanaosma elimu ya Sekondari madarasa tofauti tofauti nje ya kata hiyo ambapo shule iliyo karibu kwa sasa ni umbali wa zaidi ya kilometa 40 ina kidato cha kwanza pekee wakati shule nyingine iko umbali wa kilometa 80 kutoka kambikatoto hivyo ujenzi wa shule hiyo ni ukombozi wa kielimu wa wananchi wa kata ya Kambikatoto kwa ujumla.

Mafundi wako eneo la kazi wakiendelea na shughuli za kupaua majemngo mbalimbali shule ya sekondari Kambikatoto

Wanaonekana wakitembea karibu na jengo hilo ni wajumbe wa kamati Fedha, Uongozi na Mipango wakitembelea Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Kambikatoto

Baadhi ya Majengo yanayojengwa Kambikatoto kwaajili ya Shule Mpya ya sekondari Kambikatoto inayotaraji kuanza kuchukua wanafunzi mwaka 2024

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.