• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

VIJANA CHUNYA WAENDELEA KUPATA NEEMA KUTOKA DSW.

Imewekwa: January 21st, 2025

Vijana Vinara kupitia  mradi wa afya na maendeleo ya Vijana (REST) unaotekelezwa na shirika la DSW  wamejengewa uwezo juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ikiwa ni pamoja na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu, pamoja na mikopo ya wajasiriamali wadogo au machinga ili kuwawezesha vijana kujiajiri pamoja na kujipatia kipato kitakachowawezesha kujipatia kipato kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kuchangia katika kuinua uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Fursa hizo zimeelezwa na Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Chunya  Bi Marietha Mlozi leo tarehe 21/01/2025  wakati wa kikao cha  ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mradi wa REST kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Omary City Wilayani Chunya.

“Serikali yetu ina fursa kwaajili ya vijana kwahiyo niliona ni vizuri hadhara hii itambue fursa hizo, kwanza tuna mikopo ya yasilimia 10% kwaajili ya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu lakini pia mikopo ya wamachinga au wajasiriamali wadogo kwani mbali na kufanya shunguli za mradi ni vizuri makafahamu fursa zilizopo muweze kuzitumia lakini pia muweze kuwa mabalozi wazuri kwa vijana wengine kule mnakotoka”. Amesema Mlozi

Aidha Bi Marietha emewaeleza vijana hao vitu muhimu vya kuzingatia  ili vijana waweze kupata fursa hizo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi, kusajili kikundi lakini pia wajumbe watatakiwa kuwa na namba za nida pamoja na muhitasari wa  kikundi na mambo mengine ili kuweza kukidhi vigezo vya kupata mkopo pamoja na fursa zingine.    

Awali akizungumza mbele ya wajumbe Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la DSW linalotekeleza mradi wa afya na Maendeleo ya Vijana ndugu Peter Owaga amesema mbali na kufanya ufuatiliaji na thinini ya hali ya utekelezaji, vijana vinara wamejengewa uwezo juu ya namna ya kuandaa mpango kazi  utakao wasaidia katika utekelezaji wa shughuli zao katika jamii pamoja na kufikia malengo ya mradi

Aidha Owaga amewataka vijana vinara wa mradi kuhakikisha mambo mbalimbali waliyojifunza ikiwa ni  pamoja na kuwezeshwa kuzitambua fursa mbalimbaliza, mikopo kwa vijana na mambo mengine, kuhakikisha elimu hiyo inawafikia na watu wengine wakiwepo vijana katika maeneo yao wanayotoka kwani moja ya kazi yao ni kufikisha elimu wanayoipata kutoka kwa shirika na wadau katika jamii yao.

Naye Afisa kutoka divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Elizabeth Lusale amewaeleza vijana juu ya uwepo wa Mkopo wa wajasiriamali wa dogo au wamachinga ambapo amesema kuwa kigezo kikubwa cha kupata mkopo huo ni kitambulisho cha ujasiriamali ambacho hutolewa na Halmashauri ya Chunya ambapo kima cha chini cha mkopo huo ni shilingi laki moja (100,000) na ukomo wa mkopo huo ni shilingi million nne (4,000,000).

Wakizungumza kwa niaba ya viajana vinara wengine ndugu Yohana Kilua, Rose mwalukasa kutoka kata ya Chokaa na Obed Elia kutoka kata ya Matundasi wameuliza  juu ya watu wanaopaswa kuunda kikundi na endapo kikundi kimechukua mkopo alafu miongoni mwa wanakikundi wakawa wametangulia mbele za haki  kunakuwa na utaratibu gani  ambapo majibu ya maswali hayo yameweza kujibiwa na Maafisa Maendeleo ya jamii  ili kuwajengea uelewa vijana hao.

Kikao cha Tathimini ya mradi wa Afya na maendeleo ya Vijana (REST) unaotekelezwa na shirika la DSW kimehusisha wadau wanaotekeleza Miradi katika maeneo tofauti tofauti, wafanyakazi kutoka shirika la DSW, na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya pamoja na vijana vinara kutoka kata sita (6) za mradi ambazo ni Matundasi, Makongolosi,  Lupa, Mafyeko, Choka na Sangambi. Kikao hicho  kimeenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya michezo ambavyo ni jezi na mipira kwa vijana vinara

Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii  Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi akielezea uwepo wa fursa mbalimbali kwa vijana wakati wa kikao cha tathimini  ya utekelezaji kupitia mrari wa afya na maendeleo kwa vijana REST kilichoketi ukumbi wa Omary City.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la DSW akizungumza na vijana Vinara wa mradi  juu ya ya hali ya utekelezaji wa shughuli za mradi wakati wa kikao cha tathimini kilichofanyika Ukumbi wa Omary City Uliopo Wilaya ya Chunya.

Yohana Kilua kutoka kata ya Chokaa akiuliza swali kwa afisa maendeleo ya jamii ili kuoneza uelewa juu ya fursa mbalimbali walizoelekezwa kwaniaba ya vijana vinara wengine.

Vijana vinara wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkuu wa divisheni ya  Maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya wakiwa wamevaa jezi zao walizokabidhiwa na mipira kutoka shirika la DSW.

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.