Wataalamu wa idara na vitengo Wilaya ya Chunya wanufaika na mafunzo ya siku mbili ya uandaaji wa mpango wa bajeti ambayo huwawezesha kuandaa mpango wa bajeti wenye tija kwa maendeleo ya Halmashauri.
Mafunzo haya ya siku mbili ya uandaaji wa mpango wa bajeti yameanza jana Septemba 30, 2025 na yamehitimishwa leo Oktoba 1, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya(Mwanginde Hall) lengo likiwa ni kuwaongezewa uwezo wataalamu kuandaa mpango wa bajeti.
Afisa Mipango, Idara ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Nebert Gavu amesema tija iliyokusudiwa kwenye mafunzo ya siku mbili itafanikiwa kama maafisa bajeti(washiriki wa mafunzo) wataandaa mpango wa bajeti kwa wakati na kufanikisha malengo ya kila idara au kitengo husika.
Mafunzo haya yamehudhuriwa na maafisa wa idara na vitengo vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya(Mwanginde Hall).
Mwendesha mafunzo ndugu Nebert Gavu akifanya uwasilishaji wa mada mbalimbali kwenye mafunzo ya uandaaji wa bajeti kwa maafisa Bajeti
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya. Mafunzo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri (Mwanginde Hall) leo Oktoba 1, 2025
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.