• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

SIKU TATU ZAONGEZWA, NENDA UKAJIANDIKISHE

Imewekwa: October 13th, 2019

 Selemani Jafo, Waziri wa OR -TAMISEMI ameongeza siku tatu za kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika  24 11/2019. Akizungumza kabla ya kujiandikisha Kijijini kwake Kimani,Kisarawe mkoani Pwani , Waziri Jafo alisema kuongezwa kwa siku tatu hizo kumetokana na sababu mbalimbali ambazo kimsingi zimesababisha wananchi kuikosa fursa hiyo. 

Alisema kimsingi siku za uandikishaji huo zilizoongezwa kutoka leo hadi Oktoba 17, kumesabishwa na tatizo la mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na hivyo kuleta shida kwa wananchi wengi kujiandikisha. Aliitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na uwepo wa zoezi la wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyoleta dhana  kwa baadhi ya wananchi kuwa kitambulisho cha mpiga kura kitawawezesha kupiga kura katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa.

Mh.Jafo amesema “Kutokana na sababu hizo na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 na matangazo ya Serikali Na 371,372,373 na 374 ya Mwaka 2019 Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa  Serikali za Mitaa”  Jafo Alisema kutokana na kanuni hizo na changamoto zilizojitokeza Wizara yake imeona vyema kuongeza siku hizo tatu ili kuwapa nafasi wananchi kujiandikisha na hivyo kutumia fursa yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka. Aidha alisema tangu kuanza kwa Oktoba 8 hadi Octoba 12 Mwaka huu wananchi zaidi ya Milioni 11 walikuwa tayari wamejiandikisha nchi nzima kushiriki uchaguzi huo huku akilitaja zoezi hilo kuwa lenye mafanikio makubwa ikilinganishwa na kipindi kingine chote. Alisema kufuatia mabadiliko, ratiba ya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na matukio yanayohusu uandikishanji yatakuwa na mabadiliko fulani fulani ikiwemo kubandikwa kwa orodha ya wapiga kura litakalofanyika kuanzia Oktoba 18, utoaji wa pingamizi kuhusu uandikishaji wapiga kura litakalofanyika Oktoba 14 hadi 24. Mabadiliko mengine ni pamoja na uamuzi kuhusu pingamizi litalofanyika kuanzia Oktoba 24 hadi 25,marekebisho ya orodha ya wapiga kura kuanziaa Oktoba 25 hadi 25 pamoja na ukataji wa rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi utakaofanyika Oktoba 24 hadi 26 sambamba na ukataji wa rufaa utakaofanyika Oktoba 24 hadi 29 Mwaka huu. Aidha alisema matukio mengine yote zikiwemo kampeni za wagombea zitaendelea kubaki kama kawaida huku akiwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi huo.

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.