• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI KATIKA MTO ZILA ZAPIGWA MARUFUKU.

Imewekwa: February 14th, 2025

Shughuli za uchimbaji madini zilizokuwa zikifanyika katika mto Zila uliopo kata ya Ifumbo Wilayani Chunya zimesimamishwa mpaka pale tamko lingine litakapotolewa na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde, na kwa yeyote atakae fanya shughuli yoyote katika mto Zila hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali za   na zake pamoja na kuchukuliwa hatua zingine za kisheria.

Katazo hilo limetolewa leo tarehe 14/2/2025 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero ikiwa ni maelekezo kutoka kwa Waziri wa Madini  mpaka pale yatakapo tolewa maelekezo mengine.

“Kuanzia leo tarehe 14/2/2025 shughuli zote  za uchimbaji ndani ya mto zila zinasimamishwa rasmi kwa kampuni  ya G.&I  Mining Company Limited na kwa mtu mmoja mmoja mpaka pale waziri mwenye dhamana atakapo toa maelekezio mengine , kwamana hiyo serikali zote za vijiji , kijiji cha ifumbo  na kijiji cha Lupamaketi tunatakiwa tusimamie zoezi hili.”amesema Michombero

Aidha amewaagiza wenyeviti wa vijiji  vyote viwili , kijiji cha Ifumbo na Kijiji cha Lupamaketi  kuhakikisha wanaitisha mikutano yay a hadhara katika vijiji vyao kwaajili ya kuwajulisha wananchi wao juu ya katazo hilo la kufanya kazi za uchimbaji au shughuli zozote katika mto zila  mpaka pale watakapo pokea maelekezo mengine.

Nae Mwenyekiti wa Ifumbo ndugu Bahati Sinkwembe kwaniaba ya Wananchi amekiri kuyapokea maelekezo hayo kwaajili ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kufanya mkutano na wanakijiji kuwajulisha juu ya kutokufanya shughuli yoyote ndani yam to zila kwa masilahi ya wanaifumbo  Wilaya ya Chunya na Taifa kwa ujumla.

Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wengine  ndugu Ephrahim Angolile , Erasto Waya na Frank Tewa   wameuliza maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujua  nani atakae simamia tamko hilo lakini pia kujua hatima ya maeneo ya wananchi  yaliyoathiriwa na mwekezaji   ambapo maswali yote yaliyoulizwa yalipatiwa majibu papo hapo.

Tamko hilo limetolewa mbele ya kamati ya Usalama Wilaya NEMC, Afisa Mazingira wa Wilaya ya Chunya, Afisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Chunya na Maafisa wengine kutoka Ofisi ya Madini, viongozi wa vijiji na wananchi wa kijiji cha Ifumbo na Lupamaketi, Katazo hilo limeenda sambamba na katazo alilolitoa Waziri wa Madini Mhe.Antony Mavunde wakati alipofanya ziara yake katika mto zila mwishoni mwa mwezi Desemba 2024.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya   ndugu Anakleth Michombero akitoa tamko kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Madini  juu ya uchimbaji wa madini katika mto Zila uliopo kata ya Ifumbo Wilayani Chunya

Mwenyekiti wa kijiji cha Ifumbo ndugu  Bahati Sinkwembe akikiri kupokea agizo hilo  kwaajili ya utekelezaji .

Frank Tewa Mkazi wa kijiji cha Ifumbo akiuliza swali juu ya tamko lililotolewa kuhusu kutokufanya shughuli yoyote ya uchimbaji katika mto zila uliopo kata ya Ifumbo Wilayani Chunya.

Wananchi wa kijiji cha Ifumbo na Lupamarket wakisikiliza maelekezo yanayotolewa na katibu Tawala  Ndugu Anakleth Michombero  kuhusu Mto zila.

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.