• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

MKUU WA MKOA WA MBEYA AMPA HEKO MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA CHUNYA .

Imewekwa: February 11th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Zuberi Homera ampa heko Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chunya kwa kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo jengo la baba, mama na mtoto lilojengwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa kuzingatia thamani ya fedha na  usawa wa jinsia kwenye utoaji huduma.

Mhe. Homera ameyasema hayo leo Februari 11, 2025 wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili kwenye ukaguzi wa jengo la baba, mama na mtoto lililopo Hospitali ya Wilaya ya Chunya, ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Homera amekagua maendeleo ya ujenzi wa stendi mpya ya kisasa, ujenzi wa uwanja wa michezo, na ujenzi wa karavati uliopo jirani na jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

“Natoa pongezi Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya, Mwenyeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, tumefanya ziara nzuri tangu jana tulipoanza na leo ni siku ya pili tunahitimisha ziara hii, miradi imejengwa kwa kiwango cha juu sana, mafanikio ni makubwa na thamani ya fedha inaonekana, naamini kwa namna tunavyotekeleza miradi tunaenda vizuri kwa mkoa wa Mbeya” amesema Homera.

“Tunachohitaji sisi ni kuona thamani ya fedha tunapokuja kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maedneleo, nimeambiwa hapa jengo la baba, mama na Watoto limegharimu milioni 258 na ukiangalia hapa unaona kabisa jengo limekidhi viwango lakini pia jengo hili limezingatia usawa wa kijinsia ambapo wakinababa, wakinamama na Watoto wanapata huduma za afya” amesema Mhe. Homera.

Katika hatua nyingine Mhe. Homera amesisitiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na shule katika ngazi ya msingi na sekondari kuripoti shuleni kabla ya Machi 15, 2025 vinginevyo hatua kali za sheria zitachuliwa dhidi ya wazazi na walezi walioshindwa kuwapeleka wanafunzi shuleni.

“ Mpaka ikifika Machi 15, 2025, wakuu wa Wilaya wote, Wakurugenzi wote, maafisa elimua na Maafisa elimu kata wahakikishe wanafunzi wote waliopaswa kuanza masomo wawe shuleni haswa wa kidato cha kwanza” amesema Mhe. Homera.

Akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa karavati, Mhe. Homera amefurahishwa na utekelezaji wa agizo lake la ujenzi wa karavati alilolitoa Februari, 2023 wakati wa ziara ya kikazi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

“Febrauri, 2023 nilitoa agizo kwa Ofisi ya TARURA wilaya ya Chunya kujenga karavati kwaajili ya watumishi, wananchi kupita kwenye eneo hili la mto ili wakapate huduma mbalimbali kwenye jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, nimefurahi ujenzi wa karavati umeisha na umerahisisha mawasiliano kwa wananchi kupata huduma za kiserikali kwa kufika kwa urahisi ofisi ya  Mkurugenzi” amesema Mhe. Homera.

Naye Hanifa Rajabu mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya amemshukuru Rais watanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ya ujenzi wa karavati ambapo imeondoa adha ya kuvuka barabara hiyo wakati wa mvua lakini pia imesaidia kurahisisha kufika kituo cha kazi kwa wakati.

Vilevile, Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera amekagua ujenzi wa standi mpya ya kisasa ya mabasi ya Wilaya ya Chunya huku akimtaka mkandarasi kufanya kazi muda wa ziada ili kukamilisha ujenzi wa standi mwezi Juni, 2025.

“Sisi lengo letu ni kuja kuizindua standi ya mabasi ya kisasa mwezi Juni, 2025 ili wananchi waendelee kupata huduma za usafiri lakini pia mkandarasi unatakiwa kuchangia jamii(CSR) inayokuzunguka kwa kuwa serikali imekupa zabuni ya ujenzi wa standi unaogharimu Tsh. Bilioni 2.8, na tayari umeshalipwa Milioni 400 kama kianzio” amesema Mhe. Homera.

Awali akikagua mradi wa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Homera amempongeza mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kwa kazi kubwa ya ujenzi wa uwanja

“ Kazi kubwa kwenye uwanja ni uzio pamoja na sehemu ya uwanja (Pitch) na nimeambiwa mumeshagiza nyasi, ila sasa nyasi mulizoagiza muweke maboresho kuwe na jina la uwanja pamoja na kuendelea kujiunga mkono timu ya mpira wa miguu ya Ken Gold ambayo ni timu ya wanachunya” amesema Mhe. Homera.

Naye mhandisi wa Wilaya ya Chunya, Charles Kway amesema, uwanja wa mpira upo kwenye hatua nzuri ambapo nyasi tayari zimeshaagizwa na zinatarajia kufika nchini baada ya miezi mawili.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliambatana na viongozi wa chama cha Mapinduzi, viongozi wa serikali, wataalamu kutoka Mkoa na Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kutoka mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Chunya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera akikagua ujenzi wa mradi wa standi mpya ya kisasa ya Mabasi Wilaya ya Chunya. Standi mpya ya Mabasi inajengwa katika Kata ya Itewe jirani na Sheli ya LY.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa standi mpya ya kisasa ya Mabasi Wilaya ya Chunya. Standi mpya ya Mabasi inajengwa katika Kata ya Itewe jirani na Sheli ya LY.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa Uwanja mpya wa michezo wa Wilaya ya Chunya. Uwanja wa michezo unajengwa katika Kata ya Mbugani katika Wilaya ya Chunya.

Muonekano wa uwanja wa michezo wa Wilaya ya Chunya unaendelea kujengwa katika Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya.

Baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wakimsiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili kukagua mradi wa ujenzi wa Karavati.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera akifurahia jambo mara baada ya kukagua ujenzi wa Karavati liliwarahishia wananchi kupita njia kuelekea jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kupata huduma mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Hospitali ya Wilaya ya Chunya kukagua ujenzi jengo la huduma ya baba, mama na mtoto.

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.