• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

MHE. MASACHE “TABIA YA KUKAMATA WATU KWAKUWAONEA IKOME, SIPENDI WANANCHI KUONEWA”

Imewekwa: October 12th, 2023

Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka amewataka viongozi wa serikali ngazi ya vijiji na kata kuacha mara moja kuwakamata wananchi kwa kuwaonea jambo ambalo sio lengo la serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wake wakiwepo wananchi wa Chunya na Kata ya Ifumbo.


Ametoa Katazo hilo tarehe 11/10/2023 alipokuwa katika kijiji cha LupaMarket kilichopo kata ya Ifumbo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoianza mapema tarehe 2/10/2023 sambamba na hilo ameagiza kusomwa na kubandikwa hadharani taarifa za mapato na matumizi ya fedha kwa ngazi za vijiji ili wananchi waweze kujua fedha za serikali zinatumikaje pamoja na fedha wanazokuwa wamechangia wao wenyewe.


“Kukamata watu kwakuwaonea mkome mara moja, ila kama umefanya kosa ni haki yako kukamatwa na pia ni haki yako kupigwa faini. Ikitokea umekamatwa kwakuonewa nipe taarifa mimi nitachukua hatua mara moja maana sipendi wananchi wa jimbo la Lupa kuonewa Na pia kusoma na kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha za serikali na fedha walizochangia wananchi kwa lengo la maendeleo au lengo lingine lolote ni takwa la kisheria, kupitia mkutano huu nawaagiza watendaji wote wa serikali kuwasomea mapato na matumizi wananchi kutokufanya hivyo mnakiuka sheria na taratibu” Alisema Mhe Masache


Kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Jimbo la Lupa, Diwani wa kata ya Lupa Mhe. Weston S. Mpyila amesema kwa sasa changamoto ya wananchi wa kata ya Ifumbo ni ukamilishaji wa kituo cha Afya kinachojengwa kwenye kata hiyo kwani idadi ya wananchi wa kata hiyo imeongezeka sana jambo linalopelekea zahanati zilizopo kushindwa kuwahudumia ipasavyo, Pia Mhe Mpyila amekiri kupokea vitanda sita katia zahanati ya LupaMarket, kupokea fedha za ujenzi wa madarasa shule ya Msing LupaMarket pia ameishukuru serikali kuifungua barabara ya Kiwanja-Ifumbo ambapo zaidi ya shilingi milioni mia nne na hamsini zimetumika kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha changalawe.


“Tumepokea vitanda sita (6) zahanati ya Luapamerket, Jengo la wagonjwa wa nje limejengwa pale kwenye kituo cha Afya bado vitu vichache, pamoja na kuwa na zahanati mbili lakini kwasasa idadi ya wananchi wa Ifumbo imeongezeka hivyo uhitaji wa kituo cha Afya ni mkubwa sana”. Pia  Mhe Diwani wakati anatoa salamu kwenye mkutano wa Mhe Mbunge kwenye kijiji cha Ifumbo ameseme “…  wana Ifumbo kwasasa wamestaraabika hivyo hawahitaji kusukumwa sukumwa , na viongozi wa serikali ngazi ya kata na vijiji wapo hapa waendelee kutekeleza hilo”.


Kwa ruhusa ya Mhe Mbunge, akijibu kero ya wananchi ya kutozwa michango bila kupewa risiti pamoja na kutosomewa mapato na matumizi Afisa mipango wa wilaya ya Chunya kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji  Ndugu Mjanaheri Swalehe amesema ni kosa kutokusoma mapato na matumzi kwa wananchi na pia ni kosa kutokutoa risiti kwa mtu yeyote anapotoa pesa yoyote au michango mbalimbali ambayo ipi kisheria au mmekubaliana hivyo kupitia hadhara hiyo amewataka watumishi wote kwenye maeneo yao ya kazi wafuate taratibu za utumishi wa umma.


Mueda Muliemo, Michael Munis, Nichoraus Mwasinyanga na Faraja Mwasimba waliuliza maswali kwa niaba ya wananchi wengine kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Lupamarket wakati Brayson Daimon Mwasimba,Abeli Mlangali, Elia Wiston Waya na Veronica Mpilla waliwawakilisha wananchi wengine kuuliza maswali mbalimbali kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Ifumbo.


Changamoto kubwa iliyozungumzwa na wananchi wengi na kwa hisia kali ni uvamizi wa kampuni ya kichina kuchimba kwenye maeneo yaliyokazwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2018 wakati akiwa makamu wa Rais lakini pia Mkuu wa wilaya ya amekuwa akikemea mara kwa mara kupitia mikutano yake kwenye kata ya Ifumbo kuhusu kutokuchimba kwenye vyanzo vya maji ikiwepo kwenye mto Zilla lakini kwasasa  wananchi wanashangazwa kupewa mtu mwingine ambaye si mwenyeji wa eneo hilo kuanza kufanya shughuli zile zile ambazo wao wamekatazwa.


Mhe Masache amewataka wananchi wa Ifumbo kuwa watulivu wakati yeye kama mwakilishi wao anafuta suluhu ya kero hiyo ambayo imeonekana ni kero kubwa na inawaumiza wananchi wa kata ya Ifumbo huku wananchi hao wakishindwa kuelewa ni serikali ipi imeruhusu maeneo ambayo wao walikatazwa na walitii makazo hayo kwa muda mrefu kuanza kuchimbwa na mtu mwingine ambaye siye mwenyeji.


Ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa katika kata ya Ifumbo imehitimisha safari ya kutembelea kata zote 20 za jimbo la Lupa na kero mbalimbali zikipatiawa suluhu na nyingine ambazo zinahusisha mamlaka Mbali mabali ameahidi kuzishughulikia kwa wakati kulingana na uharaka wake lakini amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwani kila changamoto ya mwananchi inachukuliwa kwa uzito unaostahili

Diwani wa Kata ya Ifumbo Mh. Weston S. Mpyila akizungumza mbele ya wananchi wa Kijiji cha Ifumbo kabla ya Kumkaribisha Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasasa wakati alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wananchi wake

Afisa Mipango Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Mnajaheri Swalehe akijibu kero ya wananchi kutosomewa mapato na Matumizi pamoja na kutokua risiti mwananchi anapoa mchango au fedha zilizowekwa kisheria wakati wa mkutano wa Mbunge kwenye kijiji cha Lupamarket

Veronica Mpyilla mwananchi wa kijiji cha Ifumbo akiulizwa swali kwa Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa wakati alipofanya ziara ya kuzungmza na wananchi katika kijiji hicho

Mapokezi ya Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka kwenye kijiji cha LupaMarket wakati alipokuwa anawasili kwaajili ya Mkutano (Wananchi walitandika ngup zao kwa Umbali wa Zaidi ya Mita mia moja ili Mbunge  apite juu ya Nguo mkapa eneo la Mkutano)

Wananchi wa Kijiji cha Ifumbo wakimsikiliza Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache wakati alipowatembelea kusikiliza kero za wananchi hao

Wananchi wa Ifumbo wakiendelea kumsikilza Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.