Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Lupa Wakili Athuman Bamba amewataka wasimamizi wasaidizi wa ngazi ya kata kuhakikisha wanasoma Sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Tume Hur ya Taifa ya Uchaguzi ili waweze kutekeleza vyema majukumu yao waliyokabidhiwa kutekeleza kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye maeneo wanayotoka
Ametoa rai hiyo leo 4.8.2025 wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya kata wa Jimbo la uchaguzi la Lupa waliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Mwanginde Hall) unaopatikana Jengo jipya la utawala
“Pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika shughuli za Uchaguzi niwaombe msome na kuzielewa vyema Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uchagzui inayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili mkatekeleza majukumu yenu mliyopewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi katika maeneo yenu ya uteuzi” Amesema Wakili. Bamba.
Sambamba na maeekezo hayo Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Lupa amewapongeza washiriki wote kwa kuaminiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kutekeleza majukumu kwa niaba ya Tume huru katika maeneo yao wanayoishi huku akiwakumbusha kwamba uteuzi wao umezingatia utendaji kazi, weledi na uzalendo kwa Taifa lao hivyo wafanyekazi kama walivyoaminiwa.
Naye afisa Uchaguzi wa jimbo la Uchaguzi la Lupa Ndugu Ridhiwani Mshigati amewakumbusha washiriki kwamba kazi hii wanayokabidhiwa na Tume ni muhimu yenye kuhitaji watu makini na weledi huku akiwakumbusha kwamba weledi katika kazi zilizopita ndiyo msingi wa kuteuliwa kwao hivyo amesisitiza kuzingatia weledi wakati wote wa zoezi hili
Washiriki wa Mafunzo arobaini (40) kutoka kata zote ishirini (20) za Jimbo la Uchaguzi la Lupa wanashiriki mafunzo hayo ikiwa ni maandalizi kuelekea kutekeleza majukumu kama Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata ndani ya jimbo la Lupa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.