• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

MAELEKEZO MANNE YATOLEWA KWA BARAZA LA MAMLAKA YA MJI MDOGO MAKONGOLOSI.

Imewekwa: February 13th, 2025

Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya Afisa Tawala wa Wilaya ya Chunya Bi Semwano Mlawa  amewasilisha maelekezo manne (4)  kwa Baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha swala la ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao unaimarishwa katika maeneo yote ikiwepo ulinzi shirikishi . 

Maelekezo hayo yametolewa na Afisa Tawala akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya leo tarehe 13/02/2025 wakati wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Makongolosi la kuchagua Mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo na wenyeviti wa kamati mbalimbali katika Ukumbi wa Mama Mbwana Makongolosi Wilayani Chunya.

“Maelekezo 4 ya Mkuu wa Wilaya  kwa baraza la mamlaka  mji mdogo Makongolosi , jambo la kwanza  ni suala la  swala la usalama, jambo la pili ni  ufwatiliaji wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti Shuleni, jambo la tatu ni usimamizi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yetu na jambo la nne tukasimamie ukusanyaji wa mapato  na uratibu mzuri wa feda zinazokusanywa.” Amesema Bi Semwano 

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya Ndugu Noel Chiwanga ametoa rai kwa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi kutatua kero mbalimbali za wananchi, kuoa haki na kuwahudumia Wananchi kwani wananchi wanamatarajio makubwa sana na viongozi wao.

“Toeni haki kwa wananchi kwani wananchi wanamatamanio na matarajio makubwa sana kwenu , naomba kero mbalimbali za wananchi mkazipunguze kwa kiasi kikubwa sana, sasa isije ikawa  matarajio tofauti kwamba kuwepo kwako wewe ndio ikawa kero kwa wananchi” amesema Chiwanga

Nae Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (CHEDEMA) ndugu Yohana Mpamba ametoa msisitizo kwa baraza la mamlaka Mji mdogo Makongolosi kwenda kutenda haki kwa watu wote bila kubagua lakini pia   kuiga  mambo mazuri yanayofanywa na viongozi waliotangulia kwaajili ya maendeleo ya mamlaka na Wilaya ya Chunya kwa ujumla.

Kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu John Maholani amawasihi baraza la mamlaka Mji mdogo Makongolosi kufanyakazi kwa bidii kwaajili  kwani wana mamlaka makubwa ya katika kuiletea maendeleo  Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi  , Halmashauri ya Wilyaya ya Chunya na Taifa kwa ujumla

Nae diwani wa kata ya Matundasi Mhe . Kimo Choga  kwa niaba ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya  mbali na kuwapongeza  wenyeviti waliochagulia ametoa wito kwa viongozi hao kusimamia miongozo  na taratibu za Mamlaka pamoja na kusimamia  ukusanyaji mzuri  wa mapato  ambayo ndio dira ya maendeleo ya mamlaka ya mji mdoo wa makongolosi.

Balaza la Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi la kuchagua Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Baraza hilo  limeenda sambamba na kuchagua wenyeviti wa kamati mbalimbali za Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi limehudhuriwa na kamati ya Usalama Wilaya ya Chunya, Viongozi wa vyama vya Siasa wataalam kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Chunya na mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi.

Afisa Tawala Wilaya ya Chunya Bi Semwano Mlawa akitoa maelekezo manne ya Mkuu wa Wilaya kwa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mama Mbwana Makongolosi Wilayani Chunya.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  ndugu Noel Chiwanga akitoa salam za chama wakati wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi la kuchachugua viongozi wa baraza hilo na viongozi wa kamati mbalimbalii lililoketi katika Ukumbi wa Mama Mbwana wa Makongolosi Wilayani Chunya.

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi Ndugu Linus Mwanitega  akitoa ufafanuzi juu ya uchaguzi wa viongozi wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu John Maholani  akitoa rai kwa wajumbe wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi lililoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mamam Mbwana Makongolosi Wilayani Chunya.

Wajumbe wa baraza la Mamlaka Mji Mdogo Makongolosi wakifuatilia agenda mbalimbali za kikao wakati wa baraza la kuchagua Viongozi wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi  lililoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mama Mbwana Makonolosi Wilayani Chunya.




 

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.