• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

LETENI MAPENDEKEZO YA MIRADI NA BAJETI ZENU KWENYE KAMATI YA FEDHA

Imewekwa: January 15th, 2024

Kamati ya fedha Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupeleka bajeti zao pamoja na mapendekezo ya miradi wanayoitekeleza kwenye kamati hiyo ili kuamua kwa pamoja mradi upi uanze kuteklezwa na kwa gharama ipi mradi husika utatekelezwa kwani  Madiwani ndio wanaoishi na wananchi hivyo wana uelewa mkubwa juu ya mahitaji ya wananchi wao

Maoni hayo yametolewa na wajumbe wa kamati ya fedha, uchumi na mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya mwishoni mwa juma walipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwepo daraja la Lualaje linagharimu shilingi milioni mia mbili na kumi (210,116,000/=), Ujenzi wa daraja la Magunga kupitia barabara ya Ngwala linalojengwa kwa shilingi 178,214,000/= pamoja na mradi wa ujenzi wa Barabara ya Malangamilo yenye urefu wa kilomita 8 yenye thamani ya shilingi milioni 274,885,000/=

“Sasa tunaandaa bajeti ya mwaka 2024/2025 na nyinyi TARURA muwe mnatuletea bajeti yenu kwenye vikao vya kamati ya fedha ili na sisi tupate nafasi ya kushauri barabara ipi ipewe kipaumbele Zaidi lakini pia kuhakikisha bajeti inayopangwa inaenda sambamaba na uhalisia tunapoenda kukagua miradi” Alisema Mhe Mwanginde

Aidha kamati hiyo imeagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanafuatilia agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha barabara zinaenda kwenye maeneo ambayo miradi ya Build Better Tommorow (BBT) itatekelezwa zinafunguliwa ili kurahisisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi ili lengo la serikali la kuanzisha mradi huo litimie kama ilivyo kusudiwa

“Leo ni tarehe 12/1/2024 naomba kufikia tarehe 20/1/2024 mlete taarifa inayoonesha tayari bajeti ya kufungua barabara hizo imetengwa ili kamati hii ipate namna ya kuendelea kufuatilia utekelezaji wa suala hilo kama Mhe Rais alivyoagiza” Aliongeza Mhe Mwanginde

Akizungumza na kujibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  wilayani Chunya Mhandisi Emannuel S Kayola amesema miradi yote inaendelea vizuri lakini maoni, mapendekezo na Maelekezo ya wajumbe wameyachukua na watayafanyia kazi

Ziara ya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ipo katika ziara yake ya kawaida kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani Chunya na kamati imekagua miradi yenye thamani ya shilingi milioni 663,215,000/= ambayo  inasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  wilayani Chunya Mhandisi Emannuel S Kayola akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango wakati kamati hiyi ilipotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TARURA wilayani ya Chunya

Wajumbe wa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango wakiendelea na zoezi la Ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na TARURA ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Pichani ni wajumbe wakikagua ujenzi wa Barabara ya Malangamilo inayojengwa urefu wa kilomita 8 kutoka Barabara kuu ya Mbeya Tabora

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.