• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

HUDUMA YA UPASUAJI SI TATIZO TENA MAKONGOLOSI.

Imewekwa: February 27th, 2024

Wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi wameIshukuru  serikali ya awamu ya sita  inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapelekea vifaa tiba katika kituo cha afya cha Makongolosi kwani huduma nyingi zikiwepo za upasuaji walikuwa wanalazimika kuzifuata katika  hospitali  ya Wilaya  hivyo kwa kuletewa vifaa hivyo huduma nyingi watazipata katika kituo hicho.

Pongezi hizo zimetolewa Leo tarehe 27 Februari 2024 katika kituo cha afya cha Makongolosi kata ya Bwawani wakati walipokuwa wamekusanyika kwaajili ya kupokea vifaa tiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD) vyenye thamani ya million 212 vilivyonunuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hilda Fande , Amosi Mwazembe,  wakazi wa kata ya Bwawani mamlaka ya mji mdogo Makongolosi  kwa niaba ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mapokezi ya vifaa tiba katika kituo cha afya Makongolosi wamefurahi kwa kusogezewa huduma za afya hususani vifaa vya  upasuaji pamoja na jokofu la kuhifadhia miili ya wapendwa wao walio tangulia mbele za haki  kwasababu kipindi cha nyuma iliwalzimu kuifwata huduma hiyo katika hospitali ya Wilaya  kitu ambacho kilikuwa ni changamoto kubwa sana kwao

“Tunashukuru sana mama yetu kutusogezea huduma sisi wakinamama tulikuwa tunahangaika sana kipindi cha nyuma tulikuwa tukiondokewa na wapendwa wetu tunalazimika kupeleka Hospitali ya Wilaya ya Chunya..., Tulikuwa na changamoto kubwa kipindi cha nyuma tulikuwa  na huduma ya zahanati tu lakini kwasasa tunakituo cha afya na leo tumeletewa vifaa tiba kama jokofu la kuhifadhia miili ya wapendwa wetu wanapotutoka  tunamshukuru Mhe.Rais kwa kutujali wananchi wakei”.walisema Hilda na Amosi

Diwani wa kata ya Bwawani Mhe.Sailon M.Pashila  amemshukuru mhe. Samia Suluhu Hassani rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea vifaa tiba na kusema kuwa wananchi hawata pata adha ya kwenda mbali tena kupata huduma za afya hususani upasuaji na huduma zingine.

‘’Sasa nawaambia wananchi waondoe shaka Changamoto za kwenda kufuata huduma katika hospitali ya wilaya ya Chunya na Mbeya sasa labda kwa huduma za dharua pale itakapobidi kwani serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi  chini ya Rais Samia Suluhu Hassani inawajali wananchi wake kwa sasa   tunaomba serikali ituongeze na Watalam wa afya ili huduma ziweze kutolewa kwa wakati” alisema Mhe. Mpashila

Naye Burton Mwakisambwe  katibu Chama Cha Mapinduzi kata ya Bwawani amemshukuru Mhe Rais  kwa kuwaletea vifaa tiba na kusema kwakufanya hivyo wananchi wanajionea namna ambavyo chama cha mapinduzi kinatekeleza Ilani yake kwa kuwajali wananchi sambamba na hilo ameiomba serikali kuwaongezea watenda kazi kwani kwa sasa mamlaka Mjimdogo Makongolosi umekuwa na watu wengi

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya  ndugu Linus Mwanitega Mtendaji wa Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi amesema kuwa vifaa tiba vilivyopokelewa vinaenda kujibu matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji  pamoja na huduma ya kuhifadhi wapendwa wao kwa kuletewa jokofu la kuhifadhia miili ya wafu.

“Tumepokea vifaa muhimu kwasababu vinakwenda kujibu matatizo na hoja mbalimbali za utoaji wa huduma kwa wananchi wetu kwakweli haikuwa laisi lakini kwa juhudi za rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassani ameweza kutuletea vifaa tiba vyenye thamani ya million 212 na tunategemea kupokea vifaa vingine ambavyo vitakamisha million 300hivyo utoaji wa huduma kiyuo cha afya Makongososi utakuwa wakisasa tofauti na ilivyokuwa awali”.  Alisema Mwanitega

Awali akitoa taarifa ya upokeaji wa vifaa hivyo Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya  Mfamasia wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Edward Tengulaga  amesema kuwa vifaa vilivyopokelewa vyenye thamani ya shilling Millioni 212 ni pamoja na  Vitanda  70 vya kulaza wagonjwa, magodoro 70, Kitanda cha upasuaji , Utra sound  pamoja na vifaa vingine.

“Tumepokea vifaa hivi vyenye thamani ya million 212 kwa awamu ya kwanza lakini tunategemea kupokea vifaa vingine kabla ya tarehe 15 na tunategemea kuanza kutoa huduma za upasuaji kuanzia tarehe 15 Machi na utoaji wa huduma  nyingine unaendelea  kama kawaida kwa wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi” alisema Tengulaga

Kituo cha afya Makongolosi kimepokea  vifaa vyenya thamani ya shilingi million 212 ikiwa ni awamu ya kwanza na  kinategemea kupokea vifaa vingine kwa awamu ya pili vitkavyo kamilisha shilling million 300 zilizotolewa na  Mhe, Rais Samia Suluhu Hassani  kwaajili ya vifaa tiba katika kituo hicho.

Baadhi ya vitanda vilivyopokelewa kituo cha afya Makongolosi  kutoka bohari ya dawa (MSD)  ambapo jumla ya vitanda 70 va magodoro 70 vimepokelewa kwaajili ya kuhudumia wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi

wananchi wa kata ya Bwawani wakiendelea na zoezi la kushusha vifaa tiba vilivyoletwa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) katika kituo cha Afya cha Makongolosi 

Jokofu la kuifadhia miili ya wafu ikiwa ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyopokelewa kituo cha Afya Makongolosi kutoka Bohari ya Dawa (MSD)


Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.