• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DED CHUNYA “TUWAFICHUE WANAOTENDA MATENDO YA UKATILI KWENYE JAMII ZETU”

Imewekwa: December 10th, 2023

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Tamimu Kambona akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya amewataka wananchi kushirikiana kwa pamoja kuwafichua watu wanaotenda matendo ya ukatili katika jamii zetu ili waweze kuchukuliwa hatua   kwani kwa kufanya hivyo matendo ya ukatili yatapungua na jamii itabaki salama na kuwataka wasikae kimya wanapoona  mtu kafanya vitendo vya ukatili.

Kauli hiyo ametoa leo Desemba 10, 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi yaliyofanyika katika kijiji cha Shoga kata ya Sangambi  ambapo wilaya ya Chunya aimehitimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia

“Ndugu wananchi ni jukumu la kila mmoja wetu kupinga vitendo vya ukatili  hivyo  tunapaswa kushirikiana kwa pamoja  kutokomeza vitendo vya ukatili  lakini  pia kama mzazi umeona mwenzio anamfanyia mtoto vitendo vya ukatili na ukakaa kimya  vitendo vya ukatili havitakoma  hivyo tuwafichue wale  wote wanaofanya vitendo vya ukatili  katika jamii zetu  tusikae na adui jirani” alisema Kambona

Aidha Kambona amekea wakina baba wanaotoroka majukumu yao ya msingi jambo linalopelekea wakina mama kuwa na mziko mzito wa majukumu jambo linalopelekea ukatikli wa kijinsia kwao

“Wanawake na wasichana ndio kundi linalopitia changamoto nyingi kutokana na mgawanyo wa majukumu ya kifamilia akinababa tumekuwa tukikwepa majukumu mengi ambayo mengine tungeweza kuyafanya ndani ya familia mfano ndani ya familia tumevuna mazao baba anaamua kuyachukua na kwenda kuyauza na kumwacha mama anahangaika na familia” alisema Kambona.

Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew amesema madhara ya ukatili  ni makubwa na yanagharama kubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha au kupata maradhi hususani kwa mtu aliefanyiwa ukatili wa kingono, ukeketwaji na aina nyingine za ukatili hivyo jamii inapaswa kupinga vikali vitendo vya ukatili.

Awali akisoma risala kwa Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Chunya Bi Lightness Mbissa amesema miongoni mwa changomoto zinazowakabili ni pamoja na wazazi na walezi kumalizana  nyumbani wao kwa wao pindi matukio ya kikatili yanapokuwa yametendeka pasipo kufikishwa katika vyombo husika hali inayochangia kwa kiasi kikubwa matukio ya ukatili wa kijinsia kuongezeka katika jamii.

Kwa niaba ya wazee wa wilaya ya Chunya Mzee Mosses Zumba amesema wazee wanapaswa kukemea vitendo viovu vinavyoendelea katika jamii hasa ukatili wa kijinsia  kwani wazee wana nafasi kubwa katika jamii   hivyo  wanapaswa kutengeneza utaratibu wa kukaa na kuongelea  na kupinga vitendo vya kikatili

Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia imetamatika leo ambapo wilaya ya Chunya imehitisha katika kijiji cha Shoga kilichopo kata ya sangambi, katika kipindi cha siku kumi na sita wananchi 1029 wamefikiwa wanaume ikiwa ni  422 na wanawake 607 huku elimu mbalimbali ikitolewa kama vile elimu ya kujitambua, elimu ya ukatili na mambo mengine mengi

Wananchi wa kijiji cha Shoga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kilele cha kampeniya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoyofanyika kijijini hapo

Mganga Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dr Darison Andrew akielezea madhara ya Ukatili katika jamii wakati wa kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kijiji cha Shoga.

Mzee maarufu ndugu Mosses Zumba akiongeajuu ya umuhimu wa wazee katika kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii wakati wa kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kijiji cha Shoga

Mwenye kiti wa jumuiya ya wazazi kupitia chama cha Mapinduzi ( CCM) akitoa neno la shukurani kwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Shoga

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.