• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC MAYEKA ‘’WANAOBEZA MAFUNZO YA MGAMBO WAKAMATWE”

Imewekwa: July 29th, 2023

Mkuu wa wilaya ya Chunya  Mhe  Mayeka  Saimon Mayeka  amewataka wananchi na Viongozi kutokubeza mafunzo yanayotolewa kwa Mgambo kwani mafunzo hayo  yanawajenga vijana  kuwa wazalendo kwa nchi yao   Lakini pia watasaidia katika shughuli mbalimbali za maendelao na ulinzi  kwa jamii yao na Taifa kwa Ujumla


Kauli hiyo ameitoa 28/07/2023 wakati akifungua rasmi mafunzo ya Mgambo yanayofanyika kijiji cha Bitimanyanga kata ya Mafyeko ambapo vijana kutoka katika vijiji viwili (2) kijiji cha Mafyeko na Kijiji cha Bitimanyanga  ambapo jumla ya vijana 387 wamejitokeza katika mafunzo hayo 387 wanaume wakiwa  345  na wanawake 42


“Kubeza na kutoa kauli zisizo faa kuhusiana na mafunzo ya Mgambo ni kosa na wote watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa  hatua, Viongozi mpo hapa mnanisikia yeyote atakayetoa maneno ya siyofaa na kubeza Mafunzo haya akamatwe  kwasababu mafunzo haya yapo kwa mujibu wa Sheria  na yanafanyika Nchi nzima na yanafanyika kwa kalenda inayofanana, na ninyi vijana mliojitokeza kushiriki mafunzo ya Mgambo mmefanya uamuzi sahihi.’’ Alisema mhe Mayeka


Pia amewataka  vijana wote wanaopata mafunzo ya Mgambo kuwa makini na mafunzo wanayoyapata na kuhakikisha wanafuatilia kila hatua na kuelewa vizuri pia  kupokea maelekezo yote yanayotolewa na wakufunzi kwa vitendo kwani watajifunza  mambo mengi mazuri yanayoendana  na mabadiriko ya kidunia.


‘’Niwatake vijana wote mnaoshiriki mafunzo haya kuwa makini na kufuatilia  kwa vitendo,  msifanye  mafuzo haya kwa ulegevu na uzembe kama umekuja kupoteza muda unapaswa kubadilika,  ulivoingia uwe tofauti na utakavyo toka   kwani mtajifunza mambo mbalimbali kama masuala ya Rushwa, Usalama wa Nchi , mazingira ,matumizi ya silaha na mambo mengine mengi ili mtakapomaliza mkafanye majukumu yenu kwa ukamilifu”


Akitoa salam katika ufunguzi wa mafunzo hayo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Said Mwanginde amewataka vijana wote wanaopata mafunzo hayo kutambua kwamba wao ni wanajeshi hivyo wanapaswa kuwa wazalendo katika jamii na nchi kwa ujumla  kwani   jamii itawategemea sana kwa masuala ya ulinzi katika Jamii na katika kulijenga Taifa.


‘’Ninyi vijana lazima muwe wazalendo  na Nchi yenu  lazima mtambue mmeingia kwenye mfumo wa kuwa walinzi hivyo jamii itawategemea sana katika masuala ya ulinzi kwahiyo mjifunze mafunzo haya kwa manufaa yenu wenyewe na Taifa lenu na mtakapo fuzu mafunzo haya tunataka kuona jamii , kijiji na wilaya inanufaika na ninyi kupitia mafunzo mliyoyapata” alisema Mhe Mwanginde.


Awali akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi Mkufunzi na mshauri wa Mgambo wilaya ya Chunya Captain Mohamed Ali Omary  amesema changamoto inayokabili mafunzo hayo ni baadhi ya wananchi na Viongozi kubeza mafunzo hayo na kuwashawishi baadhi ya vijana kuacha mafunzo hayo na kusababisha baadhi ya vijana kuacha mafunnzo hayo hali inayopelekea kupungua kwa idadi ya wanafunzi .


Ufunguzi wa mafunzo hayo rasmi wa Mafunzo hayo umefanyika tarehe 28/7/2023  Na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa kata na vijiji, Viongozi wa chama cha Mapinduzi  pamoja na  Kamati ya Usalama  na mafunzo hayo  yalianza rasmi tarehe 3/7/2023   yanarataji kudumu kwa miezi minne  (4) na hufanyika kila mwaka pia ni zoezi la Nchi nzima

Baadhi ya vijana waliojitokeza katika mafunzo ya Mgambo mwaka huu wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo haya


Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.