• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC MAYEKA “HAKUNA MWANAFUNZI KUKAA CHINI AWAPO DARASANI CHUNYA”.

Imewekwa: May 24th, 2023

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amewataka walimu wanafunzi na jamii kwa ujumla kulinda miundombinu ya shule iliyoko katika Maeneo yao ikiwa ni pamoja na madawati ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na ameuagiza uongozi wa shule kwa ujumla kuwachukulia hatua wazazi ambao hawatimizi mahitaji ya watoto wao (wanafunzi)

Mhe. Mayeka ametoa kauli hiyo jana katika Shule ya Msingi  Mapongolo iliyopo kata ya Chokaa wilayani Chunya wakati akipokea Madawati Hamsini (50) yenye thamani ya Milioni tatu (3,000,000/=) kutoka Bank ya CRDB tawi la Chunya ikiwa ni sehemu ya Banki hiyo kurudisha Faida kwa wataje wake na kuungana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha Mwananchi wake wanapata huduma bora.

“Nikupongeze meneja wa banki ya CRDB kwa Madawati haya, Sio kidogo kama mwingine anaweza kufikiria, Ni mengi sana kwani yanatusaidia kupunguza uhitaji na hata yangekuwa madawti matano bado ningefika kuyapokea. Mkoa wa Mbeya tumekubaliana hakuna mwanafunzi yeyote anakaa chini hivyo ninyi mnatusaidia Chunya kutekeleza Mpango wetu”

Meneja wa banki ya CRDB tawi la Chunya Bw. Hamis Mbinga amesema wao Kama Banki wataendelea kuungana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali kama walivyofanya maeneo mbalimbali yakiwepo Elimu, hivyo kutoa madawati hayo hamsini (50) ni mwendelezo wa kile ambacho wamekuwa wakikifanya mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chunya

“Tumekuwa na utaratibu wa kufanya mambo tofauti tofauti kama elimu, afya na mengine ili na sisi tutoe mchango kwa jamii. Tumekuwa tunashirikiana na Mkurugenzi na Ofisi yako Mhe Mkuu wa wilaya, na katika sekta hii ya Elimu tumetoa madawati kiwanja sekondari, tumeshiriki kutengeneza maabara Kiwanja sekondari na pia kata karibu zote za tarafa ya Kiwanja tumezifika kwa kutoa madawati 240 hivi, na hili linaloendelea hapa ni mwendelezo katika kuhakikisha tunailetea maendeleo wilaya yetu” Meneja CRDB

Naye Diwani wa kata ya Chokaa Mhe. Samwel Komba kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo ameishukuru benki ya CRDB kwa namna ambavyo wameweza kutoa msaada huo wa madawati katika Shule ya Msingi Mapongolo huku akiomba kutokuwachoka pale watakapopeleka maombi mengine kwaajili ya miradi mingine ya Maendeleo

“Nikupongeze sana Meneja na endelea kupambana na sisi kama wawakilishi tuko tayari kufanya kazi na CRDB, tutakuja tena ofini kwenu hata kama sio kwa madawati kwa njia nyingine tutawafikia CRDB msituchoke, kwa niaba ya wananchi wa kata ya Mapogolo tunashukuru sana” Mhe. Diwani

Katibu wa Chama cha Mapinduzi tawi la Mapogolo Ndugu Jumanne Rashid Mariatabu akitoa salamu za Chama hicho amesema Ilani ya chama cha Mapinduzi inasimamiwa vizuri na inatekelezwa ipasavyo na viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi tawi hivyo naye ametoa shukrani kwa Meneja wa banki ya CRDB kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa Mbeya kuhakikisha wananchi wanapata elimu kwa uzuri kwani Madawati hayo yatasadia wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapongolo kusoma kwenye mazingira rafiki.

Awali akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa wilaya, Makamu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Frank Sanga amesema Shule ilikuwa na upungufu wa madawati 257, hivyo ongezeko hilo litasaidi kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo la uhaba wa madawati katika shule hiyo, huku akisema madawti hayo yatasaidia wanafunzi kusoma kwa utulivu, kuwa na mwandiko mzuri na kuleta hamasa katika kusoma.

Pamoja na kupokea Madawati hayo Mkuu wa wilaya ya Chunya amekagua ujenzi wa Madarasa mawili yanayojengwa  kupitia mradi wa Boost katika Shule ya msingi Mapogolo, huku Mhandisi wa Halmashauri  Eng Charles Kwai anayesimamia ujenzi wa mradi huo amesema mwezi juni, 2023 ujenzi wa madarasa hayo utakuwa umekamilika na kuanza kutumiwa na wanafunzi.

Picha Mbalimbali katika tukio la Makabidhiano 


Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.