Waziri wa madini Mhe. Antony Mavunde amelipokea ombi la Wakuu wa Wilaya kutoka katika Wilaya ya Chunya na Wilaya ya Songwe juu ya kuongeza kufanya utafiti wa madini katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hizo ili kuongeza uzalishaji wenye tija katika sekta hiyo na hatimae kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kukuza pato la Taifa kwa ujumla
Ombi hilo limetolewa na Wakuu wa Wilaya kwa Waziri wa Madini tarehe 03/04/2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa shughuli za uchimbaji wa madini wa Porcupine North unaofanywa na kampuni ya Shanta Gold mining Company LTD .
“Ombi la Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga na Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Solomon Itunda nimelisikia juu ya kuongeza utafiti wa madini katika meneo mbalimbali ili kuongeza tija ya serikali katika kupata mapato kupitia sekta hii ya madini, Waheshimiwa wakuu wa Wilaya nakubaliana nanyi hatuwezi kuiendeleza sekta ya madini pasipo kufanya utafiti wa kina kwasababu utafiti ndio moyo wa ukuwaji wa sekta ya madini” alisema Mhe. Mavunde
Aidha Mhe. Mavunde ameongeza kuwa Mhe Rais aliwaongezea bajeti sekta ya madini na kiasi kikubwa cha bajeti hiyo kimeelekezwa katika kufanya utafiti wa kina kwa lengo la kukuza sekta kwani imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pesa za kigeni na kukuza pato la Taifa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga mbali na kutoa ombi la kuongeza utafuti wa madini katika maeneo mbalimbali pia ameishukuru kampuni ya Shanta Gold Mining kwa kuanza Shughuli za uchimbaji kwani kupitia kampuni hiyo wazawa watajipatia ajira lakini pia wachimbaji wengine watapata ujuzi kupitia kampuni hiyo na serikali kujiongezea mapato na hatimaye kukuza uchumiwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Awali akitoa salam za Chama Mwenye kiti wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Noel Chiwanga ametoa rai kwa mwakezaji kutumia fursa kwa tija kubwa lakini pia kuhakikisha wazawa wanakuwa kipaumbele katika kufanya kazi mbalimbali katika kampuni hiyo ili na wao waweze kunufaika na uwekezaji huo
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Shanta Ndugu Honest Mrema Akisoma taarifa kwa Mgeni rasimi amesema kuwa lengo la kampuni ni kuendelea kufanya utafiti wa kina kwenye maeneo yote ya leseni ili kuongeza maisha ya mgodi kwa miaka mingi ijayo na kwa mwaka huu wa 2025 Kampuni imetenga zaidi ya billioni 12 kwaajili ya utafiti wa madini kwenye eneo la Lupa ili kukuza shughuli za uzalishaji wa madini Nchini.
Akiongea kwa niaba ya wachimbaji wadogo Ndugu Abraham Mwakyalagwe Ameishukuru serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kukuza sekta ya madini na kuwapigania wachimbaji wadogo huku akitoa ombi juu ya uboreshwaji wa miundo mbinu ya barabara pamoja na ujenzi wa Soko kubwa la kisasa katika Wilaya ya Songwe.
Uzinduzi wa shughuli za uchimbaji wa Madini katika mradi wa Porcupine North umehudhuriwa na , waziri wa madini , Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya kutoka Mbeya na Songwe Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya na Mkoa , wafanyakazi wa Shanta Gold Mining , Viongozi wa mila na Wananchi wanao zunguka aneo la mgodi ,
Waziri wa madini Mhe. Antony Mavunde akizungumza na hadhira wakati wa hafla ya uzinguzi wa shighuli za uchimbaji madini wa porcupine North unaofanywa na kampuni ya Shanta Gold Minging Wilayani Chunya.
Viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Mbeya na Songwe wakishuhudia Waziri wa madini akikata utepe kuashiria rasmi kuanza kwa shughuli za Uchimbaji wa madini mradi wa porcupine North .
Mkuu wa Wilaya ya Chunya upande wa kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Songwe upande wa kulia wakiwa wameambatana na Waziri wa madini Mhe Antony Mavunde alievaa kofia pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Shanta Gold Mining.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Shanta Gold Mining baada ya hafla ya uzinduzi wa shughuli za uchimbaji mradi wa Porcupine North
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.