• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC CHUNYA AWAKEMEA WATUMISHI WANAOTUMIA MUDA WA KAZI KWA SHUGHULI BINAFSI.

Imewekwa: September 19th, 2023

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewakemea watumishi wanaotumia muda wa serikali kufanya shughuli zao binafsi jambo linalopelekea kushuka kwa tija ya utumishi na utendaji wao kwani wanaoathirika ni Wananchi wanaotakiwa kuhudumiwa na watumishi katika maeneo mbalimbali ya wilaya

Ametoa kauli hiyo tarehe 18/9/2023 katika ukumbi wa mikutano Sapanjo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vilivyotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maafisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ili kurahisisha utendaji kazi wao na baadaye kuleta Tija kwa wananchi na Tanzania kwa ujumla wake .

“Tutagombana mkiacha kufanya kazi za serikali mkaegemea kazi zenu binafsi muda wa kazi, Hivyo Nendeni mkafanye kazi vinginevyo mvivu ataonekana tu. Serikali inachotaka toka kwenu ni Tija yaani uwepo wako afisa kilimo na afisa mifugo uonekane kupitia kazi sio wakulima wanalima bila tija, wafugaji wanafuga bila tija na wewe upo tu maeneo hayo sasa kazi yako ni nini?” alisema Mhe. Mayeka

Mhe ,Mayeka amemtaka mkuu wa divisheni ya Kilimo na Mifugo wilaya ya Chunya kuandaa vigezo vya kuwapima maafisa hao na kuandaa ziara ya kukagua maeneo yao ya mfano kwani ni vigumu afisa mifugo kutokuwa na mifugo na hata afisa kilimo kutokuwa na shamba, hivyo ameagiza kuandaliwa kwa ziara maalumu ya kupita kukagua mifugo na mashamba ya maafisa hao

“Tutaandaa ziara maalumu ya kupita kukagua shamba la afisa kilimo lisilopungua heka moja pamoja na kukagua mifugo kwa afisa mifugo maana haiwezekana afisa kilimo hauna shamba na afisa Mifugo hauna mifugo” alisema Mhe. Mayeka

Naye Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Ndugu Cuthberth Mwinuka akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya amesema zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo ni mwendelezo wa serikali kuwasaidia maafisa hao ili kutekeleza majukumu yao jambo ambalo litaleta tija kwa mwananchi moja kwa moja kwani awali serikali iligawa vifaa vya usafiri kama vile Pikipiki lakini leo imeendeleza zoezi hilo kwa kuleta vifaa vingine

“Zoezi hili Mhe Mkuu wa wilaya ni mwendelezo kwani awali serikali ilitupatia vyomba vya usafiri ili kurahisisha maafisa hawa kufika maeneo mbalimbali ya kazi lakini sasa imetuongezea vifaa vingine ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Majukumu yetu ya kila siku” alisema Ndugu Mwinuka

Afis kilimo kata ya Sangambi ndugu Raymond Choga na Afisa ugani kata ya Matundasi  ndugu Shani Ngoma kwa niaba ya wenzao wameishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyowajali huku wakiahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi katika maeneo yao na kwa kufanya hivyo wanasema waatakuwa wametimiza azma ya serikali

Vifaa vilivyogawiwa kwa maafisa kilimo na mifugo  kwa kata zote za wilaya ya Chunya ni pamoja na Buti, koti, Pumpu Kompyuta, printa pamoja na kipima udogo (Soil scanner) Tableti pamoja na karatasi Maalumu (Transparency).

Mkuu wa Wilaya Mhe. Mayeka akimkabidhi buti ,  koti la mvua na pamp Afisa kilimo wa kata ya Maundasi ndugu Shani Ngoma

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka  aliesimama katikati kwenye picha ya pamoja na maafisa  kilimo na mifugo wa kata za halmashaui ya Chunya


Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.