• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC BATENGA: “SHULE ZOTE CHUNYA ZIWE NA MASHAMBA YASIYOPUNGUA HEKARI 10”

Imewekwa: February 16th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga  ameagiza Shule zote wilayani Chunya kuwa na Mashamba yasiyopungua hekari kumi ili mazao yatakayopatikana yatumike kama chakula kwa wanafunzi jambo ambalo litawaondolea  wazazi na walezi  mzigo wa kuchangia huku akiagiza Maafisa Ugani kusimamia Mashamba hayo vizuri ili kuwawezesha wananchi wengine kuja kujifunza mbinu  mbalimbali za kilimo chenye manufaa.

Maagizo hayo ameyatoa leo wakati aliposhiriki kikao cha kamati ya Lishe cha Robo ya pili kwa mwaka 2023/2024 kilichoketi leo tarehe 16/2/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya uliopo jengo jipya la utawala.

“Tunakwenda kutengeneza mashamba darasa katika shule zetu zote wilayani Chunya. Shule ziwe na Mashamba yasiyopungua heka kumi (10) na mazao yanayopatikana yatumike kwaajili ya chakula shuleni na maafisa ugani wa kata wasimamie mashamba hayo, Kwakufanya hivyo lile lengo la kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika utekelezaji wa mkata wa Lishe litafanikiwa” Amesema Mhe Batenga

Katika nafasi nyingine amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa juhudi kubwa anazofanya katika kusimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe ambapo kupitia juhudi hizo wilaya ya Chunya kw mara tatu mfululizo imeshika nafasi ya tatu kitaifa katika utekelezaji wa mkataba wa Lishe

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona amewataka Idara tumizi na simamizi kwa ujumla kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa afua za lishe zinatumika kama ilivyokusudiwa kwani yeye katika ofisi yake ni kuhakikisha fedha zinapatikana lakini kazi ya kusimamia iko chini ya Idara zinazohusika kutumia na kusimamia fedha hizo

“Hatutaki taarifa za mwisho zinakuja zinaeleza eneo Fulani tuna asilimia 99.9 au asilimia chini ya hapo, sisi tunachotaka kila eneo kama miongozo inavyoelekeza tunafikia asilimia 100 na kama tunaruhusiwa hata Zaidi lakini sitaki kuona tuko chini ya asilimia 100 eneo lolote la utekelezaji wa mkataba wa Lishe, naomba idara simamieni hili”

James Sunge kaimu Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii, Mw Abdalah Mchelu kaimu mkuu wa idara ya elimu ya Awali na Msingi, Mw Konzeta Ngachenga kaimu mkuu wa idara ya elimu Sekondari na Nicholaus Chambala kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya pili pamoja na mikakati yao kuhakikisha kile kilichokusudiwa kinafikiwa kwa wakati na kwa weledi

Kikao cha kawaida cha kamati ya lishe wilaya ya Chunya kimeketi leo tarehe 16/2/2024 kikiwa na lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe kwa Robo ya pili jambo ambalo hutoa dira juu ya kinachoendelea kufanyika katika kipindi cha Robo ya tatu ikiwa ni pamoja  na kurekebisha panaoonekana kukwamisha utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.

Afisa lishe wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka akifafanua jambo wakati wa kikao cha Lishe Robo ya pili ya mwaka 2023/2024 kilichoketi mapema leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo jengo jipya la utawala Halmashauri ya wilaya ya Chunya

Mganga mkuu wa wilaya ya Chunya Dr Darison Andrew akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa mwaka ulipopita mbele ya Mkuu wa wilaya mapema leo wakati wa kikaao cha Lishe robo ya pili ya mwaka 2023/2024

Kaimu mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu James Sunge akijibu hoja wakati wa kikao cha kamati ya Lishe baada ya kumaliza kuwasilisha taarifa ya idara hiyo juu ya utekelezaji wa afua za Lishe

Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu ya awali na Msingi wilaya ya Chunya Mw Abdalah Mchelu akifafanua namna ambavyo idara itahakikisha agizo la shule la kuwa na mashamba namna litakavyotekelezwa katika idara ya Elimu ya awali na msingi

Kaimu mkuu wa Idara ya Elimu sekondari Mw Konzeta Ngachenga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe zilizofanywa na Idara ya elimu sekondari kwa Robo ya pili ya mwaka 2023/2024

Wajumbe wa kamati ya Lishe wakiwa kwenye kikao cha Lishe kwa Robo ya pili ya mwaka 2023/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo Jengo jipya la Halmashauri ya wilaya ya Chunya

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.