• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC BATENGA, “MAAFISA MAENDELEO WOTE MKAWE WALEZI WA VIKUNDI VILIVYOKOPESHWA."

Imewekwa: January 31st, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Chyunya Mhe.Mbaraka Alhaji Batenga amewataka Maafisa Maendeleo ya jamii kuwa walezi wa vikundi vilivyokopeshwa na Halmashauri  katika maeneo yao ili kuweza kuvifuatilia kwa karibu  kujua vinafanya nini na kufanya tathimini kila robo ili kuona mwenendo mzima wa mkopo huo unaendaje , na kama kunachangamoto yoyote itakayopelekea kikundi kushindwa kurejesha mkopo huo kuweza kuitatua changamoto hiyo mapema .

Kauli hiyo ameitoa Mhe.Batenga leo Tarehe 31/1/2025  wakati wa hafla ya  kukabidhi Hundi ya Shilingi  Millioni 803, 200,000 kwa Vikundi 83 vya Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo)

“ Maafisa maendeleo ya jamii wote kwenye maeneo ambayo vikundi hivi vimechukua mkopo  ninyi mkawe walezi wa vikundi hivi , lazima muwe na ratiba ya mwaka mzima ya kupitia vikundi hivi na kuvifanyia tathimini ili kama kunakikundi kinataka kwenda vibaya kisaidiwe mapema kabla mambo hayajaharibika natujue tunafanya nini, kwahiyo nawakabidhi ninyi kwa maafisa Maendeleo ya jamii wakawe walezi wenu.” alisema Mhe. Batenga

Aidha Mhe. Batenga  ametoa msisitizo kwa vikundi vyote vilivyokopeshwa kuhakikisha vinarejesha Mkopo huo kwa wakati ili kuviwezesha ni vikundi vingine kunufaika na mkopo huo wa asilimia 10% unaotolewa na  Halmashauri  kupitia mapato yake ya ndani  kwani ni mkopo usio kuwa na riba yoyote ,kikundi kinarejesha tu kiasi cha Mkopo uliokoposhwa.

Naye mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde ametoa rai kwa vikundi kutokukopa kwa kufuata mkumbo bali wakope fedha hizo kwaajili ya kufanyia shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara pamoja na shughuli zingine za kuwaongezea kipato ili waweze kurejesha mkopo huo pamoja na kunufaika wao kama kikundi na  mtu mmoja mmoja na hatimae Taifa kwa ujumla.

Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi  akisoma taarifa kwa mgeni rasmi amesema kuwa  vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kabla ya kupewa mikopo hiyo wamewajengewa uwezo juu ya usimamizi wa vikundi, usimamizi na uendeshaji wa miradi , utunzaji wa kumbukumbu , kuweka akiba na mambo mengine mengi yatakayo saidia vikundi hivyo viweze kujiendesha kwa ufanisi.

Goodanswer  Richard  kutoka kundi la vijana wengine  na Ernest Itelekelo  kutoka kundi la watu wenye ulemavu wakiwakilisha vikundi vilivyopata mkopo wameishukuru serikali ya Dkt samia suluhu Hassan kwa kurudisha tena mkopo wa asilimia 10% unaotolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwani mkopo huo hauna riba tofauti na mikopo inayotolewa na taasisi zingine , Lakini pia wamewasihi wenzao waliopata mkopo huo kurejesha kwa uaminifu ili waweze kuaminika na kukopeshwa tena wakati mwingine.

 Hundi ya shilingi Millioni 803,200,000 imetolewa kwa vikundi vya wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu  ikiwa ni asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo vikundi  vya wanawake ni 41, vikundi vya vijana 38 na vikundi vya watu wenye ulemavu 4  kwa awamu ya kwanza  na awamu ya pili ya kuomba mikopo yenye thamani ta shilingi million 1,260180.53 itaanza tarehe 10/12/2025.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akiwafunda wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi millioni 803,200,000.

Mmwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde akiwasihi vikundi vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu kuwa waaminifu katika kurejesha mkopo waliopewa na Halmashauri wa asilimia 10.

Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii  Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi akisoma taarifa kwa mgeni rasmi wakati wa  hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi millioni 803,200,000 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akiwakabidhi hundi ya shilingi millioni 803,200,000 vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kataika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri (Sapanjo).


Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • TARAFA YA KIPEMBAWE CHUNYA YAJIDHATITI KUWATUMIKIA WANANCHI.

    March 21, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.