Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewataka wakulima wa vyama vya ushirika wilaya ya Chunya kuhakikisha wanamiliki ardhi kwaajili ya matumizi ya sasa na hata matumizi ya baadaye ya vyama hivyo kwani ardhi inaongezeka thamani kila siku
Ametoa kauli hiyo mapema leo tarehe 14/05/2025 katika kijiji cha kalangali wakati akifungua rasmi kiwanda cha kusaga Unga na kukamua mafuta ya alizeti mali ya Chama Kikuu cha Ushirika cha wakuima wa Tumbaku Chunya (CHUTCU)
“Hata ninyi wenyewe mnaongoza wakulima ambao wana ardhi hivyo hata ninyi vyama vya ushirika hakikisheni mnamiliki ardhi na mkishakuwa na ardhi hakikisheni mnatafuta hati, hakuna kitu kinatafutwa kwasasa kama ardhi, jambo hili ni muhimu sana hapo mbeleni. Wekeni ardhi hiyo salama kwakuikatia hati ili kiongozi atakayekuja na anauchu na ardhi asiweze kuitafuna” amesema Batenga
Aidha Mhe Batenga amevitaka vyama vtote wananchama kuongeza juhudi ya kulima mahindi na Alizeti ili kuhakikisha kiwanda hicho kinapata malighafi za kutosha jambo ambalo kwanza linawatea wakulima faida kwakuwa soko la mahindi la uhakika lipo lakini faida itakayotokana na uzalishaji wa unga wa kutosha na kuuza huku akihimiza kuongeza juhudi ya kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo.
“Vyama vya msingi wekeni utaratibu wa kuona namna ambavyo mtalisha kiwanda hiki ili malighafi ziwepo maana kiwanda kina uwezo wa kufanyakazi masaa ishirini na nne hivyo kwa kuwepo malighafi za kutosha kutasaidia kiwanda kuzalisha kwa kiwango stahiki na hatimaye mtapata faida zaidi” ameongeza Mhe Batenga.
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Mbeya Bwana Richard Edlia amesema ufunguzi wa kiwanda hicho ni tafsiri ya moja kwa moja ya Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ya kuongeza thamani mazao ya wakulima kwani kiwanda hiki moja kwa moja kitaongeza thamani ya Mahindi na alizeti za wakulima wa wilaya ya Chunya.
Awali akitoa taarifa za ujenzi wa kiwanda hicho Bwana Fransisco Chidege amesema lengo la ujenzi wa kiwanda hicho ni kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima wa Mahindi na Alizeti wa wilaya ya Chunya kwa kupata eneo la kuuza mazao yao kwa bei nzuri jambo ambalo litaendelea kuwanufaisha na kuongeza uchumi wa mkulima mmoja mmoja na hatimaye uchumi wa Taifa kwa ujumla
Hafla ya ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusaga unga wa Mahindi na kukamua mafuta ya Alizeti kilichogharimu shilingi milioni mia nne sitini na saba imefanyika leo ambapo Mkuu wa wilaya ya Chunya alikuwa mgeni rasmi. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka vyama vyote vya msingi vilivyopo mkoa wa kitumbaku Chunya pamoja na wananchi wa karibu na eneo kilipo kiwanda hicho.
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Mbeya Bwana Elia Richard akitoa neno wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa kiwanda
Bwana Fransisco Chidege (Mhasibu wa CHUTCU) akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kiwanda mbele ya Mgeni rasmi mapema leo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga (Kulia) akisikiliza Msomaji akisoma kibao kinachoonesha maandishi hapo ukutani naada ya kufungua rasmi kiwanda hicho
Unga unaozalishwa kwenye kiwanda kilichofunguliwa rasmi leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.