Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga ahimiza tija kilimo cha Tumbaku kwa vyama 27 vya msingi vya kilimo cha Tumbaku Wilaya ya Chunya.
Akizungumza na vyama vya ushirika vya kilimo cha Tumbaku katika kikao cha tathmini cha kuanza msimu mpya wa Kilimo cha Tumbaku katika Ukumbi wa chama cha ushirika cha Lupa(LUPA AMCOS) leo Oktoba 17, 2025 amesema ni vyema vyama vya ushirika kuzingatia kanuni na masharti ya kilimo cha Tumbaku ili kuongeza tija ya zao hilo muhimu ambalo linamchango mkubwa kwa Uchumi wa Wilaya ya Chunya na wananchi.
“Tunapomaliza msimu wa kilimo ni muhimu kufanya tathmini kujua msimu umekwendaje na kupata picha ya tunapoelekea. Niwapongeze wakulipa kwa kuliheshimisha zao la Tumbaku, sisi ni miongoni na Wilaya zinaongoza kwa uzalishaji wa kilimo cha Tumbaku na zao hili linaipa hadhi Wilaya ya Chunya kuitwa Mkoa wa Kitumbaku, tunashindana na Mikoa na Wilaya zinazozalisha Tumbaku” amesema Mhe. Batenga.
Aidha, Mhe. Batenga amewataka wakulima kuzingatia utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti ikiwa ni takwa la sheria ambalo linahalalisha uuzwaji wa Tumbaku pamoja na kuwahimiza wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuendelea kuzingatia kilimo bora na ushauri wa kitaalamu kwenye matumizi sahihi ya mbolea, kudhibiti upotevu wa majani ya Tumbaku na kuepuka kufanya kilimo maeneo yaliyozuiliwa ikiwemo maeneo ya hifadhi ya misitu na vitalu vya uwindaji.
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya ununuaji Tumbaku (Premier), Fred Sau amesema kampuni ya Premier inazingatia suala la Uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti sambamba na kulipa ushuru na kuchangia kwa jamii kutokana na mapato yanayopatikana katika kila msimu wa kilimo cha Tumbaku.
“Suala la uhifadhi wa mazingira ikiwemo kwa kupanda miti tunalizingatia, tumeboresha majiko kwa kutumia mfumo wa (zigzag channel). Vilevile tumelipa ushuru Tsh. Milioni mia tatu na hamsini kwa Halmashauri, pia tunachangia milioni 39 kwa jamii kwenye miradi ya iliyolenga kilimo, afya na mazingira pamoja na utawala bora.
Kampuni ya Mkwawa nayo ilisisitiza wakulima kuzingatia masharti ya uzalishaji zao la Tumbaku kwa kutowahusisha watoto katika kilimo cha Tumbaku na wanyakazi wanaotoka nje ya nchi kuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.
Akijibu swali lililoulizwa na Upendo Mwabukusi mkulima wa Lyeselo AMCOS akitaka kujua kwanini wanalipa bima na wanapopata majanga ikiwemo mvua ya mawe hawapati fidia kwa wakati, Meneja wa benki ya NMB Tawi la Chunya, Rasul Msangi amesema benki ya NMB hupeleka fedha ya fidia ya majanga kwa Kampuni ya Bima ambayo hulipa wakulima moja kwa moja.
“Bima zinalipa wakulima wanaopata majanga ikiwemo mvua za mawe kwa mfano AMCOS ya Muungano wamelipwa japo hawajalipwa kama inavyotarajiwa, AMCOS ya Lyeselo tayari tumeshapeleka kwa Kampuni ya bima ya UAP ila bado hawajalipa. Kama benki tutachukua hatua ya kuona namna ya kushughulikia suala la bima kwa wakulima wa Tumbaku” amesema Mvungi.
Wakulima wa vyama vya msingi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga katika kikao cha tathmini ya zao
la Tumbaku kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa LUPA AMCOS, Chunya.
Mkulima wa chama cha msingi LYESELO(LYESELO AMCOS) Upendo Mwabukusi akiuliza swali kwa kampuni ya ununuaji Tumbaku katika kikao
cha tathmini ya zao la Tumbaku kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa LUPA AMCOS, Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.