• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DAS CHUNYA, TUMIENI MBAO ZILIZO KAUKA KUTENGENEZA SAMANI ZA MIRADI HII

Imewekwa: October 13th, 2023

Katibu Tawala wilaya ya Chunya ndugu Anackleth Michombero  amewataka na kuwasisitizia wasimamizi wa miradi ya SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement) kuhakikisha shamani zinazotumia mbao kama vile milango na madawati  zitengenezwe kwa mbao zilizokauka vizuri ili  zisipoteza ubora wa Mradi  kwani wakitumia mbao mbichi zitakapokauka  zinaweza kupasuka na kupoteza ubora wa thamani hizo.

Ametoka kauli hiyo jana terehe October 12, 2023 wakati alipotembela na kukagua miradi hiyo katika kata ya Lualaje na Kambikatoto na kujionea halihalisi ya  ujenzi inavyoendelea ambapo mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kambikatoto upo hatua ya upauaji wakati mradi wa Ujenzi wa nyumba ya walimu (2 in 1) upo hatua ya upauaji na upigaji wa plasta.

Pia Katibu tawala amewapongeza wasimamizi wa miradi ya SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement) kwa hatua ya ujenzi wa miradi ilipofikia katika ujenzi wa Shule ya Sekondari kambikatoto wenye thamani ya Shilingi Milioni miatano themanini na tatu (583.180.028) pamoja na Ujenzi wa nyumba ya walimu yenye uwezo wa kubeba familia mbili (2 in1) katika shule ya Sekondari Lualaje yenye thamani ya shilingi milioni miamoja (100.000.000).

‘’Nawapongeza sana kwa hatua hii ya ujenzi mliyofikia mmefanya kazi nzuri hongereni sana  lakini mjitahidi kukimbizana na muda kwa hatua zilizobaki  ili kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati  huku mkiendelea kuwashirikasha wananchi kwa sehemu ambazo mnahitaji nguvu za wananchi” alisema Michombero

Naye Afisa elimu Vifaa na takwimu halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Costansia Komba amepokea maelekezo ya katibu tawala na kuwataka wasimamizi wa ujenzi walioko eneo la miradi hiyo kuhaikisha wanawatembelea mara kwa mara wazabuni wao ilikuhakiki ubora wa malighafi zinazotumika kutengenezea thamani za milango na madawati.

Awali akisoma taarifa Afisa elimu kata wa kata ya Kambikatoto ndugu Msana Mahona amesema kuwa kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa mpaka sasa imechangiwa na nguvu kubwa ya wananchi ambapo ni pamoja na kusafisha eneo la ujenzi, kulipa fidia eneo la ujenzi, kubeba mchanga, kokoto, mawe na kifusi   mbayo ni sawa na million 45,035,000 na kuongeza kuwa wananchi bado wanaendelea kushiriki katika ujenzi wa mradi huo.

 Nae afisa elimu kata wa kata ya Lualaje ndugu Evaristo Kayeta amesema kuwa wananchi wameshiriki katika mradi huo kwa kiasi kikubwa ambapo jumlaya million 10,914,000 ni nguvu ya wananchi iliyotumika mpaka hatua ya mradi ulipofikia sasa nabado wananchi wanaendelea kujitolea nguvu kazi mpaka mradi utakapokamilika.

Katika kutembelea na kukagua miradi ya SEQUIP Katibu tawala pia alitembelea shule mpya ya Kipembawe iliyojengwa katika kijiji cha Mafyeko kata ya Mafyeko kupitia mradi wa BOOST ambapo ujenzi wa Shule hiyo umekamilika yamesalia mambo madogomadogo ambayo wanaendelea kuyakamilisha.

Katibu tawala  Ndugu Anakleth Michombero akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Kambikatoto iliyopo kata ya Kambikatoto akiwana  na baadhi yawasimamizi wa mradi huoBaadhi  ya majengo ya madarasa Shule ya Sekondari Kambikatoto kupitia mradi wa SEQUIP

Nyumba wa walimu shule ya Sekondari Lualaje   iliyojengwa kupitia mradi wa SEQUIP yenye jumla ya vyumba 6 ikiwa na uwezo wa kubeba familia mbili (2 in 1)  

Katibu Tawala aliyekaa dawati la kwanza upande wa kulia  kwenye picha ya pomoja na baadhi ya wasimamizi wa mradi wa BOOST  Shule mpya ya msingi Kipembawe iliyojengwa kata ya Mafyeko walipokuwa wakikagua madawati hayo

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.