• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

CHUNYA YAENDELEA KUTAFUTA MWAROBAINI WA KULINDA WANYAMAPORI, VIUMBE HAI NA KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Imewekwa: September 1st, 2024

Shirika la TDFT chini ya mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili kwa ufadhiri wa watu wa Marekani wamefanikisha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi sitini (60) wa Shule za Msingi na Sekondari zenye kutoka tarafa ya Kipembawe wilayani Chunya zenye Klabu za Uhifadhi wa wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa mazingira kwa ujumla (TAWA MALIAHAI KLABU) kwenda kujifunza uhifadhi wa wanyamapori, viumbe hai na utunzaji wa Mazingira katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Akifafanua kuhusu ziara hiyo meneja wa mradi Ndugu Samson Ipyana Mwakihaba amesema lengo la ziara hiyo ni kuwafundisha kwa vitendo wanafunzi wanachama wa klabu za uhifadhi wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa Mazingira kwa ujumla ili kwanza kuthibitisha walichojifunza kwa nadharia lakini pia kuongeza uelewa juu ya uhifadhi, na baadaye kuandaa mabalozi sahihi na wenye uelewa sahihi wa uhifadhi wa wanyama pori, viumbe hai na utunzaji wa mazingira kwa ujumla wake

“Tuko kwenye ziara kwa lengo la kuongeza elimu kwa vitendo juu ya Uhifadhi wanyapori, viumbe hai na mazingira kwa ujumla huku Lengo likiwa ni kuandaa mabalozi wazuri wa uhifadhi wa wanyama pori, viumbe hai na  utunzaji wa Mazingira kwa ujumla na bila shaka watakuwa walimu wazuri kwa watu wengine hususani jamii inayowazunguka hivyo lengo la kuongeza Elimu juu ya uhifadhi wa wanyamapori, viumbe hai na utunzaji wa mazingira litakuwa limefanikiwa” Amesema Mwakihaba

Aidha Mwakihaba pamoja na kuishukuru Serikali ya Marekani kufadhiri mradi huo uliopelekea wanafunzi kupata ziara ya mafunzo kwa vitendo, pia ametaja Shue zilizonufaika na ziara hiyo ya mafunzo Shule ya Sekondari Mtanila (wanafunzi 10), Shule ya Msingi Matwiga (Wanfaunzi 10) Shule ya Msingi Mafyeko (wanafunzi 10), Shue ya Msingi Bitimanyanga (wanafuzni 10), Shule ya Msingi Kambikatoto (wanafunzi 10) na Shule ya Msingi Sipa (wanafunzi 10) hivyo kukamilisha idadi ya wanafunzi 60. Walimu wane kutoka Sipa, Matwiga, Bitimnyanga na Mtanila waliungana ili kuwasimamia wanafunzi hao

 

Afisa kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya ambaye alikuwa mmojawapo katika Safari hiyo Bi Jennifer  Oscar amesema safari inafaida kubwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwani pamoja na kuongeza uelewa wa washiriki katika mambo ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira amesema wanafunzi wamepata burudani, wameongeza kuifahamu jiografia ya nchi yao hivyo kuendelea kukuza uzalendo ndani ya mioyo yao lakini inaongeza hamasa kwanza kwa washiriki wa safari na baadaye wanafunzi wengine nao watahamasika kushiriki kwenye uhifadhi wa mazingira wakijua iko siku nao wataenda kujifunza maeneo mengine mbali na nyumbani kwao

Ziara hiyo imedumu kwa siku tatu ambapo Martha Marko kutoka Shule ya Sekondari Mtanila, na Shabani Brown kutoka Shule ya Msingi Matwiga kwaniaba ya wanafunzi wengine wamesema wamefurahia safari hiyo huku wakishuhudia wanyama mbalimbali kwa ukaribu tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwani kila kitu ilikuwa nadharia kwao na kupitia ziara hiyo wanafunzi wamekiri kuenda kuitumia vyema elimu waliyoipata ili kuhakikisha wanyamapori na viumbe hai wengine wanakuwa salama katika maeneo yetu

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.