• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

CHUNYA YAENDELEA KUSAKA VYANZO VINGINE VYA MAPATO

Imewekwa: December 19th, 2023

Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia viongozi wake imeanza mchakato wa kufanya biashara ya Hewa Ukaa ili kuongea uwezo wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuingiza mapato na hatimaye kuendelea kuongoza katika ukusanyaji wa mapato ndani ya Mkoa lakini kuendelea kutekeleza miradi ya Maendeleo yenye lengo la kusogeza huduma kwa wananchi wa Chunya ili waendelee kuifurahia serikali ya awamu ya sita

Katika kutimiza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mh. Bosco S. Mwanginde ameongoza msafara wa Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipngo kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ambayo tayari ni mnufaika wa Biashara hiyo ambapo mpaka sasa miradi mbalimbali ya maendeleo imejengwa kwenye wilaya hiyo kutokana na biashara ya hewa ukaa (Biashara ya Kaboni)

Katika ziara hiyo iliyohusisha waheshimiwa Madiwani wajumbe wa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango (FUM) pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ililenga kupata ufahamu wa kina kuhusu mchakato mzima wa Biashara ya Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) na baadaye kuona  namna ambavyo Halmashauri ya wilaya ya Chunya itaweza kujihusisha na biashara hiyo ambayo pamoja na kujipatia fedha lakini pia itaongeza usimamizi na utunzaji wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya

Miradi iliyotekelezwa kwa fedha zitokanazo na biashara ya Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) Keiyer Ilikiush Afisa Mipango na uratibu ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya WMA “Kadiri miaka inavyoongezeka ndivyo kaboni inavyozidi kuongezeka na kadiri Kaboni inavyoongezeka ndivyo wilaya ya Kiteto inavyozidi kupata faida

Kupitia fedha hizo miradi mbalimbali katika wilaya ya Kiteto imetekelezwa huku wanaofaidika zaidi ni vijiji wenye mradi

   -Madarasa zaidi ya 17 yamejengwa katika vijiji vitatu kupitia fedha zinazotokana na Biashara ya Hewa ukaa (Kaboni)

    -Nyumba ya walimu ya Mbili katika moja (Two in one) imejengwa kupitia fedha hizo

    -Jengo la Mama na Mtoto lenye hadhi ya kituo cha Afya limejengwa kwenye zahanati ya kata ya Makame

     -Ofisi ya Kijiji cha Kata vimejengwa kwa fedha za hewa ukaa

      -Bweni lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 kwenye shule ya sekondari ya tarafa  ya Makame limejengwa kwa fedha za hewa ukaa

       -Zaidi ya wanafunzi 200 kutoka maeneo ya mradi wamesomeshwa kwa kufadhiliwa na fedha zinazotokana na  mradi huo

       -Maabara za kisasa zimejengwa kwenye vituo vya Afya kupitia fedha zitokanazo na mradi Hewa ukaa (Mradi wa Kaboni)

       -Ofisi za kata na vijiji hupata fedha za kuendeshea ofisi kutoka kwenye mradi Hewa ukaa (Mradi wa Kaboni)

Diwani wa kata ya Makame Mhe Issaya Kilaye Ndutui amewashauri viongozi na msafara mzima toka wilaya ya Chunya kwamba kabla ya Biashara hii kuanza kuingiza fedha ni muhimu mpango wa matumzi ya fedha hizo ukawekwa ili fedha zikipatikana ni kuendelea kutekeleza mpango husika jambo hilo husaidia uwazi wa matumzi ya fedha

Naye diwani wa kata jirani na Makame Mhe Paulo Yohana Laizer amesema kupitia mradi wa biashara ya Hewa Ukaa kila kijiji wamenunuliwa dume bora la Ng’ombe, wamepatiwa Milioni tabo ambazo ni nje ya mkataba, wananchi mia moja kutoka kila kijiji kinachonufaika na mradi wa Biahsra ya Hewa ukaa wamelipiwa Bima ya Afya hivyo amewashauri kamati ya fedha Uchumi na Mipango kuenda kuona namna bora ya kuingia kwenye biashara hii kwani inafaida nyingi kwa wananchi

Mhe Ramadhani Shumbi, Mh. Weston S. Mpyila, Mh. Phide K. Mwalukasa ni baadhi ya waheshimiwa Madiwani waliouliza Maswali Mbalimbali wakati upande wa wataalamu, Dkt Lucas Theodory, Bi Simphrose Kavishe na wengine pia waliuza Maswali mbalimbali na kupatiwa ufafanuzi na wataalamu kutoka wilaya ya Kiteto

Baada ya Mafunzo na maelekezo ya Baishara ya Hewa ukaa (Biashara ya Kaboni) Mwenyekiti waHalmashauri ya wilaya ya Chunya kwa Niaba ya msafara Mzima aliwashukuru wenyeji wa kata ya Makame na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa namna walivyowapokea lakini pia kwa elimu waliyowapatia pia aliwataka kuendelea kuwa wavumilivu pale Chunya itakapowahitaji kwa maelekezo na mahusiano zaidi wasisite kuwasikiliza na kuwasaidia

Biashara ya Hewa Ukaa nini basi?

Biashara ya Hewa ukaa wakati mwingine Huitwa Biashara ya Kaboni ambapo mtu binafsi, kijiji, Halmashauri na taasisi nyingine yoyote inaweza kuanza kupata kuingiza fedha kwa kuamua kutenga msitu na kuutunza kiasi cha kusaidia kupunguza hewa mbaya (Carbon dioxide) inayopatikana huku angani

Kupitia Biashara hiyo Halmashauri ya wilaya ya Kiteto imepata faida tofauti tofauti ambapo kwa kila mwaka kiwango cha fedha wanachopata huongezeka kutokana na uwezo wa kutunza na kutokukata miti katika misitu tengwa kuendelea kuimarisha mfano mwaka

                                     -2020/2021 walipata Milioni sitini (60)

                                    -2021/2022 walipata bilioni moja na milioni miatatu

                                    -2022/2023 wamepata bioni mbini na milioni mia tano

Biashra hii imeshaingia katika Mikoa mbalimbali ikiwepo mkoa wa Katavi, wilaya ya Tanganyika ambapo wananchi zaidi ya 21,000 katika vijiji 8 walio katika Halmashauri ya Tanganyika wamenufaika na mradi wa hewa ukaa baada ya kuvuna hewa hiyo na kupewa kiasi cha shilinmi milioni mia tatu na themanini elfu (380,000,000/=)

Walichofanya wananchi katika wilaya hiyo ni kuzuia uharibifu wa mazingira katika misitu waliyoihifadhi ili iwasaidie kuvuna hewa ya kaboni na hatimaye kujiingizia kipato baada ya hewa iliyovunwa kuuzwa/kufidiwa na makampuni kutoka nje ya Nchi

Kwa ufafanuzi zaidi vijiji hivyo kutoka Halmashauri ya Tanganyika vimevuna jumla ya tani 82,000 za hewa ya kaboni na kuiuza kwa thamani ya shilingi milioni mia mbili na hamsini (250,000,000/=) hata hivyo pamoja na uvunaji watani hizo, mauzo yake hayajafikia hata nusu ya tani laki mbili na sabini (270,000/=) ambazo bado hazijauzwa

Aidha mwaka 2020 zaidi ya shilingi milioni mia moja na thelasini zilitolewa kwa viji wanufaika wa mradi  kama motisha na wadau mbalimbali wa mazingira ambazo ni nje ya makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Tafiti zinaeleza kwamba katika vijiji hivyo vya wilaya ya Tanganyika kuna utajiri mkubwa wa misitu hivyo kama itasimamiwa vizuri kuna uwezekano wa kupata pesa zaidi ya bilioni sita (6,000,000,000/=) kutokana na biashara ya hewa ukaa

Mkoa wa Iringa pia uko katika biashara hii ya hewa ukaa ambapo vijiji vinne  kutoka wilaya ya Mufindi vilipata milioni mia mbili na themanini mwaka 2021 kutokana na biashara ya hewa ukaa(Biashara ya kaboni) ambapo fedha hizo zilisaidia maendeleo ya wananchi katika vijiji hivyo. Vijiji vilivyonufaika na fedja hizo ni Kijiji cha Uchindilele shilingi milioni 140, Kijiji cha Mapanda shilingi milioni 67.4, kijiji cha Chogo Shilingi Milioni 64.4 na kijiji cha Kitete shilingi milioni 8.4

Swali linabaki kwako Mwananchi wa Chunya 

  • Kwa misitu inayozunguka wilaya ya Chunya, tutavuna kiasi gani cha Fedha kama tukiamua kuingia katika Biashara ya Hewa Ukaa???
  • Je tutashindwa kuhifadhi mazingira (kutokuta miti) ili tupate fedha za kujengea miundombinu Mbalimbali ya maendeleo?

Endelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika wilaya ya Chunya akisaidiwa na viongozi kama vile  Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya na vyombo vyake, Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mhe Bosco S Mwanginde, Watendaji wa serikali wakiongozwa na Ndugu Tamimu Kambona Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

Elimu kuhusu biashara ya hewa ukaa itaendelea kukufikia kupitia mitandao yetu ya halmashauri ya wilaya ya chunya

Lazaro C. Rinjano afisa Maliasili wilaya ya Kiteto akitoa salamu za ukaribisho kwa msafara wa Waheshimiwa Madiwani wajumbe wa kamati ya FUM pamoja na viongozi  mbalimbali kutoka wilaya ya Chunya walipowasili Halmashauri ya wilaya ya kiteto

 

Diwani wa kata ya Ndedo Mhe Paulo Yohana Laizer akifafanua jambo mbeya ya Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati msafara kutoka wilaya ya Chunya ukiwasili makao makuu ya mradi wa WMA tayari kupata elimu kuhusu Hewa ukaa (Kaboni). Misitu inayoonekana kuzunguka eneo hilo ndiyo aina ya misitu ambayo huwapatia faida kupitia hewa ukaa (Biashara ya Kaboni)

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco S Mwanginde akitoa salamu za wilaya ya Chunya kwa viongozi wa Wilaya ya Kiteto (Hasa Eneo la Mradi) na akifafanua lengo la safari hiyo kwenye wilaya ya Kiteto

Diwani wa kata ya Makame (Eneo ambalo linaendesha mradi wa Hewa ukaa) Mhe Issaya Kilaye Ndutui akifafanua jambo kwa viongozi toka wilaya ya Chunya kabla ya kuanza mafunzo kuhusu Elimu ya Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) na namna inavyowanufaisha wananchi wa kata hiyo

Afisa mipango wilaya ya Kiteto ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Bodi ya mradi wa WMA Ndugu Keiyer Ilikiush akitoa Elimu kuhusu mradi wa Hewa Ukaa (Biashara ya Kaboni) na namna wilaya ya Kiteto ilivyofaidika tangu walioanza kutekeleza mradi huo

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Ramadhan Shumbi (Aliyesimama na amenyoosha mikono mbele) akiuliza jambo kuhusu Hewa ukaa huku akieleza namna alivyokuwa anaelewa kuhusu Hewa Ukaa kabla ya kupatiwa mafunzo

Diwani viti maalumu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mh. Phide K. Mwalukasa akiuliza swali kuhusu aina ya misitu inayohusika kwenye mradi na pia ulazima wa misitu kuwa eneo moja 

Diwani wa kata ya Ifumbo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mh. Weston S. Mpyila akiuliza swali la uelewa wakati wa mafunzo kwa viongozi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya yanayohusu biashara ya Hewa ukaa (Biashara ya Kaboni)

Katibu tawala wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero akifafanua jambo wakati wa mafunzo kuhusu Hewa ukaa wakati wa ziara ya viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kujifunza Wilayani Kiteto

Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Lucas Theodory akiuliza jambo wakati wa Mafunzo kuhusu biashara ya Hewa Ukaa (Biashara ya kaboni) wakati wa Ziara ya Mafunzo wilayani Kiteto

Bi Simphrose Kavishe mtaalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya akihoji jambo wakati wa Mafunzo kuhusu Hewa Ukaa wakati viongozi wa wilaya ya Chunya walipotembelea wilaya ya Kiteto ili kujifunza kuhusu Hewa Ukaa

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.