Kikao cha tathimini ya lishe ngazi ya kata kimezimia shule zote kuhakikisha zinatoa chakula kwa asilimia 100% kwa wanafunzi wawapo shuleni ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya ufwatiliaji wa mara kwa mara shuleni lakini pia kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Kuhakikisha kila shule imelima mazao ya chakula kwaajili ya kurahisisha upatikanaji wa Chakula Shuleni ili kuwapunguzia gharama wazazi za kuchangia chakula .
Anakleth Michombero katibu tawala Wilaya ya Chunya akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ametoa azimio hilo leo tarehe 25/02/2025 wakati wa kikao cha Tathimini ya lishe ngazi ya kata cha robo ya pili kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Mwanginde Halmashauri ya Wilaya ya Chunya jengo jipya la utawala.
‘’Moja ya maazimio ya kikao hiki ni kuhakikisha kila shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inatoa chakula kwa asilimia 100% ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya ufwatiliaji wa karibu katika shule hizo , lakini pia niwaombe twendelee kushirikiana kkuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri katika masuala ya lishe ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi maeneo yenye mapungufu’’ amesema Michombero
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dk Zuberi Mzige ametoa rai kwa wajumbe wa kikao hicho kwendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu pamoja na kuendelea kutoa Elimu ya kwa jamii kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa huo wa Kipindupindu na Magonjwa maengine ikiwepo ugonjwa wa Maburg.
‘’Ugonjwa wa Kipindupindu bado ni vita katika maeneo yetu niwaombe tuendelee kuchukua tahadhari lakini pia pigeni marufuku watu kunywa maji ya kwenye mito kwasababu maji hayo yamepimwa yameonekana si salama , lakini pia Ikitokea kuna mtu kafia nyumbani asizikwe mbaka mbaka chanzo cha kifo kijulikane “ alisisitiza Dr Zuberi.
Vile vile Mganga Mkuu amewataka watendaji kufuatilia zahanati bubu pamoja na maduka ya madawa ambayo yamefunguliwa bila utaratibu katika maeneo yao na kutoa taarifa ili waweze kufanya ufwatiliaji na kuwawajibisha wahusika hao kwani wanatoa huduma pasipo kufuata taratibu na miongozo ya wizara ya afya.
Kaimu Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala ameendelea kusisitiza juu ya kampeni ya serikali ya kuhakikisha taasisi zote zinatumia nishati safi hivyo kuwataka watendaji kwendelea kujipanga kuona namna ya kutekeleza kampeni hiyo lakini pia kuhakikisha Shule zinajenga store kwaajili ya kuhifadhia chakula na majiko ya kupikia.
Aidha ameongeza kuwa kitengo cha lishe kwa mwaka wa fedha 2026/2026 wametenga bajeti kwaajili ya mashine za kuongeza virutubishi kwenye nafaka ambapo wataanza na kata tano za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambazo ni Makongolosi, Chokaa, Lupa ,Ifumbo, na Chalangwa ili kwendelea kutatua changamoto za lishe .
Kikao cha Tathimini ya lishe ngazi ya kata cha robo ya pili kimehusisha idara ya Afya, elimu msingi na sekondari, Mipango na uratibu , utumishi, watendaji wa kata na waratibu wa lishe ngazi ya kata ambapoma mbo mbalimbali yamejadiliwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shule zinatoa chakula kwa asilimia 100%. Kwa wanafunzi wawapo shuleni.
Wajumbe wa kikao cha tathimii ya lishe ngazi ya kata robo ya pili wakipitia na kujadili agenda mbalimbali za kikao hicho kilichoketi katika ukubi wa Mikutano wa Hamashauri ya Wilaya ya Chunya (Mwaninde hall)
Kaimu Afisa lishe Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala akielezea mpango wa bajeti kwaajili ya mashine za kuongeza virutubishi katika nafaka
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.