• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

CHUNYA KUINGIA 10 BORA KITAIFA UKUSANYAJI WA MAPATO

Imewekwa: April 18th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamim H Kambona amesema wilaya ya Chunya imejipanga kuhakikisha inakuwa katika Halmashauri Kumi bora katika ukusanyaji wa Mapato kitaifa kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 jambo ambalo linawezekana kwani kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 Halmashauri ya wilaya ya Chunya imevuka lengo la Makusanyo kwa Zaidi ya asilimia 140 mpaka April.

Amesema hayo Mapema leo tarehe 18/04/2024 ofisini kwake wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema Chunya inafanya vizuri katika utekelezaji wa Majukumu yake kwasababu ya Ushirikiano uliopo wakati wa utekelezaji wa Majukumu hayo.

 “Tunataka kuingia kwenye 10 bora za ukusanyaji wa mapato kitafa,  mbali na kwamba tumeendelea kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya lishe  kwa sushika nafasi ya tatu kitaifa mara tatu mfululizo, Utoaji wa Chanjo  kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa  na katika  utoaji wa huduma za  Mpango wa  Taifa wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa”. Amesema Kambona

Aidha Kambona amesema kuwa Halmashauri ya wilaya  ya Chunya imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na maeneo mengine kutokana na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watumishi wote ,  Baraza la Madiwani pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri hali iliyopelekea Chunya kwendelea kufanya vizuri katika ngazi ya kimkoa na kitaifa kwa ujumla.

“Halmashauri inafanya vizuri maeneo mbalimbali kutokana ushirikiano mkubwa uliopo kwa waumishi wa Halmashauri kwa ujumla wake, Baraza la Madiwani, Kamati ya usalama, wadau wa Maendeleo na wananchi wote kwa ujumla, na tunaendelea kuimarisha ushirikiano kwa watumishi wote bila kujali daraja la mtumishi ili kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri Zaidi”. Ameongeza Kambona

Pia Kambona amesema Halmashauri Itaendeleo kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri  pamoja na  kuongeza vitendea kazi kwa watumishi  wote ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi ili hatimaye lengo la Serikali ya awamu ya Sita la kuwarahisishia wananchi wake upatikanaji wa huduma liendelee kutimia Chunya

Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inatarajia kukusanya shilingi bilioni nane kwa mapato ya ndani mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo mwaka 2023/2024 Halmashauri itakiwa kukusanya Shilingi bilioni 5.5 lakini mpaka Aprili 5 Halmashauri imekusanya Shilingi bilioni 7.9 ambayo ni asilimia 143 ya makadirio yaliyowekwa mwaka 2023/24.




Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.