• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

AFISA ELIMU MKOA WA MBEYA AWAFUNDA WALIMU WILAYANI CHUNYA

Imewekwa: May 13th, 2024

Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwalimu Kiduma Mageni amewafunda walimu wa Shule za Msingi na awali wilayani Chunya kwakuwambia lazima wayapende mazingira yao ya kazi kwani muda mwingi wa Maisha yao hutumia kuwepo mazingira ya Shule na kwakuyapenda Mazingira hayo itavutia walimu kufundisha lakini itavutia wanafunzi kusoma kwa bidii

Ametoa maelekezo hayo mapema leo tarehe 13/05/2024 wakati akizungumza na walimu wakuu, walimu wakuu wasiaidizi ,Maafisa elimu Kata pamoja na walimu wa taaluma kwenye kikao kilichoketi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) kikoa chenye lengo la kuendelea kuimarisha ufundishaji wa wanafunzi ili kufikia lengo la kufanya vizuri kwenye mitihani ya ndani na ya nje

“Hakikisheni pale shuleni ni sehemu ya kuishi hivyo mazingira yawe yenye kuvutia na pia ongezeni ubunifu katika kufanya mazingira ya Shuleni yanakuwa yenye kuvutia lakini ubinifu katika ufundishaji wa Masomo ili kuhakikisha wanafunzi katika Shule zenu wanafanya vizuri”amesema Mageni

Mwalimu Mageni pia amewataka uongozi wa Shule kwa maana ya Mkuu wa Shule, Mwalimu Mkuu msaidizi pamoja na Mtaaluma kuhakikisha wanawajali walimu na watumishi wengine waliopo katika shule zao, kwakufanya hivyo kila mmoja atajituma katika kutekekeleza majukumu yake jambo litakalosaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wao.

“Wakuu wa Shule na viongozi wa Shule kwa Ujumla hakikisheni mnawajali walimu na watumishi wengine wanaofanyakazi chini yenu, Kwa kufanya hivyo mtawafanya wajitume katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku jambo litakalopelekea ufaulu stahiki katika shule husika, hivyo wakati mwingine kufeli ni kuamua tu”amesema Mageni

Aidha Mwalimu Mageni ameongeza kuwa kila Shule kupata ufaulu asilimia mia inawezekana endapo kila mwalimu atasimama katika nafasi yake na kujituma ikiwa ni pamoja na walimu wakuu kuwajua walimu wao na masomo yao wanayofundisha lakini pia kujiwekea malengo na kuhakikisha yanatimia .

Naye Afisa elimu awali na msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu Ferd Y. Mhanze ametoa rai kwa Walimu kuhakikisha  maelekezo yote na maagizo kutoka kwa Afisa elimu wa Mkoa  wanakwenda kuyafanyia kazi kwaajili ya kuhakikisha Chunya inafanya vizuri katika taaluma  

Kikao cha Afisa elimu Mkoa wa Mbeya kimehusisha  Maafisa elimu Msingi kutoka Wilayani, Maafisa elimu kata, Walimu wakuu, Walimu wakuu wasaidizi,Walimu wa Taaluma, Mdhibiti ubora, na afisa TSC  lengo likiwa ni kujadili mambo mbalimbali katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inafanya vizuri  katika taaluma kwani Chunya Bila Kufeli Inawezekana.

Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwalimu Kiduma Mageni akizungumza na walimu wakati wa kikao chake kilichoketi leo tarehe 13/05/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)

Afisa Elimu awali na Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalim Ferd Y Mhanze akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Afisa Elimu Mkoa na walimu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)

Walimu wa Shule za awali na Msingi wakiendelea kufuatilia Kikao na aliyesimama Mbele akizungumza ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Mwalimu Kiduma

Chunya bila kufeli inawezekana, Walimu, viongozi na wananchi tushirikiane kuhakikisha watoto wetu wanafanya vizuri

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • WAZIRI MCHENGERWA AWATAKA MAAFISA HABARI KUTOA TAARIFA SAHIHI KWA WANANCHI

    May 23, 2025
  • MAMA NA MWANAYE WAKABIDHI DAWATI 41 SHULE YA MSINGI MATWIGA, CHUNYA

    May 19, 2025
  • DC BATENGA, "HAKIKISHENI MNAMILIKI ARDHI"

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.