Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka Saimon Mayeka amesema kuwa upotevu wa mapato ni jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Halmashauri hivyo waheshimiwa Madiwani na wataalam mshirikiane katika kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya Halmashauri ikiwa ni pamoja na kudhibiti utoroshwaji wa madini na vyanzo vingine ili kuendelea kufanya vizuri zaidi katika ukusanyaji wa mapato kama ambavyo Halmashauri imekuwa ikifanya vizuri
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya wakati akitoa salam mwishoni mwa juma katika mkutano wa Madiwani robo ya kwanza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliohudhuriwa na wadau mbalimbali
‘’Vita ya utoroshwaji wa dhahabu bado inaendelea kwa kasi na vita hii si vita ya mtu mmoja niwaombe Waheshimiwa Madiwani na wataalam tushirikiane kudhibiti utoroshwaji wa dhahabu kwani unaathiri sana mapato yetu kama Halmashauri kwa kutukosesha ushuru wa huduma ( sevice levy) kwasababu ya watu wachache wasiokuwa waaminifu” alisema Mhe. Mayeka
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema kuwa miradi mingi ya Halmashauri inatekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani hivyo jitihada Zaidi zinzhitajika katika kudhibiti upotevu wa mapato ili kuiwezesha halmashauri kuendelea kufanya vizuri na kuongoza katika ukusanyaji wamapato kimkoa
‘’Niwaombe waheshimiwa Madiwani na wataalam twendelee kushirikiana katika Nyanja zote ili kuhakikisha hakuna mianya yoyote ya upotevu wa mapato ikiwa ni pamoja na kuangalia mapungufu yaliyojitokeza wakati uliopita na kuyafanyia kazi ili twendelee kufanya vizuri zaidi na zaidi katika ukusanyaji wa mapato’’ alisema Mhe. Mayeka
Nae mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ndugu Noel Chiwanga wakati akitoa salamu ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kwendelea kufanya vizuri katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukusanywaji wa mapato lakini pia usimamizi mzuri wa fedha za serikali ya awamu ya sita chini ya mhe. Rais Samia Suluhu Hassani katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mkutano wa baraza la madiwani umehudhuriwa na Mkuu wa wilaya waheshimiwa Madiwani, Wakuuwa idara mbalimbali katika halmashauri ya wiliya ya Chunya , viongozi wa chama cha Mapinduzi , wadau kutoka taasisi mbalimbali , waandishi wahabari pamoja na wananchi.
Makam Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Ramadhani Shimbi wapili kutoka kulia akiendelea kuongoza wajumbe wa mkutano wa cha la madiwani katika kuchangia mada
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.