Wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi wameIshukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapelekea vifaa tiba katika kituo cha afya cha Makongolosi kwani huduma nyingi zikiwepo za upasuaji walikuwa wanalazimika kuzifuata katika hospitali ya Wilaya hivyo kwa kuletewa vifaa hivyo huduma nyingi watazipata katika kituo hicho.
Pongezi hizo zimetolewa Leo tarehe 27 Februari 2024 katika kituo cha afya cha Makongolosi kata ya Bwawani wakati walipokuwa wamekusanyika kwaajili ya kupokea vifaa tiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD) vyenye thamani ya million 212 vilivyonunuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hilda Fande , Amosi Mwazembe, wakazi wa kata ya Bwawani mamlaka ya mji mdogo Makongolosi kwa niaba ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mapokezi ya vifaa tiba katika kituo cha afya Makongolosi wamefurahi kwa kusogezewa huduma za afya hususani vifaa vya upasuaji pamoja na jokofu la kuhifadhia miili ya wapendwa wao walio tangulia mbele za haki kwasababu kipindi cha nyuma iliwalzimu kuifwata huduma hiyo katika hospitali ya Wilaya kitu ambacho kilikuwa ni changamoto kubwa sana kwao
“Tunashukuru sana mama yetu kutusogezea huduma sisi wakinamama tulikuwa tunahangaika sana kipindi cha nyuma tulikuwa tukiondokewa na wapendwa wetu tunalazimika kupeleka Hospitali ya Wilaya ya Chunya..., Tulikuwa na changamoto kubwa kipindi cha nyuma tulikuwa na huduma ya zahanati tu lakini kwasasa tunakituo cha afya na leo tumeletewa vifaa tiba kama jokofu la kuhifadhia miili ya wapendwa wetu wanapotutoka tunamshukuru Mhe.Rais kwa kutujali wananchi wakei”.walisema Hilda na Amosi
Diwani wa kata ya Bwawani Mhe.Sailon M.Pashila amemshukuru mhe. Samia Suluhu Hassani rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea vifaa tiba na kusema kuwa wananchi hawata pata adha ya kwenda mbali tena kupata huduma za afya hususani upasuaji na huduma zingine.
‘’Sasa nawaambia wananchi waondoe shaka Changamoto za kwenda kufuata huduma katika hospitali ya wilaya ya Chunya na Mbeya sasa labda kwa huduma za dharua pale itakapobidi kwani serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassani inawajali wananchi wake kwa sasa tunaomba serikali ituongeze na Watalam wa afya ili huduma ziweze kutolewa kwa wakati” alisema Mhe. Mpashila
Naye Burton Mwakisambwe katibu Chama Cha Mapinduzi kata ya Bwawani amemshukuru Mhe Rais kwa kuwaletea vifaa tiba na kusema kwakufanya hivyo wananchi wanajionea namna ambavyo chama cha mapinduzi kinatekeleza Ilani yake kwa kuwajali wananchi sambamba na hilo ameiomba serikali kuwaongezea watenda kazi kwani kwa sasa mamlaka Mjimdogo Makongolosi umekuwa na watu wengi
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Linus Mwanitega Mtendaji wa Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi amesema kuwa vifaa tiba vilivyopokelewa vinaenda kujibu matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji pamoja na huduma ya kuhifadhi wapendwa wao kwa kuletewa jokofu la kuhifadhia miili ya wafu.
“Tumepokea vifaa muhimu kwasababu vinakwenda kujibu matatizo na hoja mbalimbali za utoaji wa huduma kwa wananchi wetu kwakweli haikuwa laisi lakini kwa juhudi za rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassani ameweza kutuletea vifaa tiba vyenye thamani ya million 212 na tunategemea kupokea vifaa vingine ambavyo vitakamisha million 300hivyo utoaji wa huduma kiyuo cha afya Makongososi utakuwa wakisasa tofauti na ilivyokuwa awali”. Alisema Mwanitega
Awali akitoa taarifa ya upokeaji wa vifaa hivyo Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mfamasia wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Edward Tengulaga amesema kuwa vifaa vilivyopokelewa vyenye thamani ya shilling Millioni 212 ni pamoja na Vitanda 70 vya kulaza wagonjwa, magodoro 70, Kitanda cha upasuaji , Utra sound pamoja na vifaa vingine.
“Tumepokea vifaa hivi vyenye thamani ya million 212 kwa awamu ya kwanza lakini tunategemea kupokea vifaa vingine kabla ya tarehe 15 na tunategemea kuanza kutoa huduma za upasuaji kuanzia tarehe 15 Machi na utoaji wa huduma nyingine unaendelea kama kawaida kwa wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi” alisema Tengulaga
Kituo cha afya Makongolosi kimepokea vifaa vyenya thamani ya shilingi million 212 ikiwa ni awamu ya kwanza na kinategemea kupokea vifaa vingine kwa awamu ya pili vitkavyo kamilisha shilling million 300 zilizotolewa na Mhe, Rais Samia Suluhu Hassani kwaajili ya vifaa tiba katika kituo hicho.
Baadhi ya vitanda vilivyopokelewa kituo cha afya Makongolosi kutoka bohari ya dawa (MSD) ambapo jumla ya vitanda 70 va magodoro 70 vimepokelewa kwaajili ya kuhudumia wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi
wananchi wa kata ya Bwawani wakiendelea na zoezi la kushusha vifaa tiba vilivyoletwa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) katika kituo cha Afya cha Makongolosi
Jokofu la kuifadhia miili ya wafu ikiwa ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyopokelewa kituo cha Afya Makongolosi kutoka Bohari ya Dawa (MSD)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.