• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

DC BATENGA AHIMIZA TIJA KILIMO CHA TUMBAKU KWA VYAMA VYA MSINGI CHUNYA.

Imewekwa: October 17th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga ahimiza tija kilimo cha Tumbaku kwa vyama 27 vya msingi vya kilimo cha Tumbaku Wilaya ya Chunya.

Akizungumza na vyama vya ushirika vya kilimo cha Tumbaku katika kikao cha tathmini cha kuanza msimu mpya wa Kilimo cha Tumbaku katika Ukumbi wa chama cha ushirika cha Lupa(LUPA AMCOS) leo Oktoba 17, 2025 amesema ni vyema vyama vya ushirika kuzingatia kanuni na masharti ya kilimo cha Tumbaku ili kuongeza tija ya zao hilo muhimu ambalo linamchango mkubwa kwa Uchumi wa Wilaya ya Chunya na wananchi.

“Tunapomaliza msimu wa kilimo ni muhimu kufanya tathmini kujua msimu umekwendaje na kupata picha ya tunapoelekea. Niwapongeze wakulipa kwa kuliheshimisha zao la Tumbaku, sisi ni miongoni na Wilaya zinaongoza kwa uzalishaji wa kilimo cha Tumbaku na zao hili linaipa  hadhi Wilaya ya Chunya kuitwa Mkoa wa Kitumbaku, tunashindana na Mikoa na Wilaya zinazozalisha Tumbaku” amesema Mhe. Batenga.

Aidha, Mhe. Batenga amewataka wakulima kuzingatia utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti ikiwa ni takwa la sheria ambalo linahalalisha uuzwaji wa Tumbaku pamoja na kuwahimiza wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuendelea kuzingatia kilimo bora na ushauri wa kitaalamu  kwenye matumizi sahihi ya mbolea, kudhibiti upotevu wa majani ya Tumbaku  na kuepuka kufanya kilimo maeneo yaliyozuiliwa ikiwemo maeneo ya hifadhi ya misitu na vitalu vya uwindaji.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya ununuaji Tumbaku (Premier), Fred Sau amesema kampuni ya Premier inazingatia suala la Uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti sambamba na kulipa ushuru na kuchangia kwa jamii kutokana na mapato yanayopatikana katika kila msimu wa kilimo cha Tumbaku.

“Suala la uhifadhi wa mazingira ikiwemo kwa kupanda miti tunalizingatia, tumeboresha majiko kwa kutumia mfumo wa (zigzag channel). Vilevile tumelipa ushuru Tsh. Milioni mia tatu na hamsini kwa Halmashauri, pia tunachangia milioni 39 kwa jamii kwenye miradi ya iliyolenga kilimo, afya na mazingira pamoja na utawala bora.

Kampuni ya Mkwawa nayo ilisisitiza wakulima kuzingatia masharti ya uzalishaji zao la Tumbaku kwa kutowahusisha watoto katika kilimo cha Tumbaku na wanyakazi wanaotoka nje ya nchi kuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Akijibu swali lililoulizwa na Upendo Mwabukusi mkulima wa Lyeselo AMCOS akitaka kujua kwanini wanalipa bima na wanapopata majanga ikiwemo mvua ya mawe hawapati fidia kwa wakati, Meneja wa benki ya NMB Tawi la Chunya, Rasul Msangi amesema benki ya NMB hupeleka fedha ya fidia ya majanga kwa Kampuni ya Bima ambayo hulipa wakulima moja kwa moja.

“Bima zinalipa wakulima wanaopata majanga ikiwemo mvua za mawe kwa mfano AMCOS ya Muungano wamelipwa japo hawajalipwa kama inavyotarajiwa, AMCOS ya Lyeselo tayari tumeshapeleka kwa Kampuni ya bima ya UAP ila bado hawajalipa. Kama benki tutachukua hatua ya kuona namna ya kushughulikia suala la bima kwa wakulima wa Tumbaku” amesema Mvungi.

Wakulima wa vyama vya msingi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Batenga katika kikao cha tathmini ya zao 

la Tumbaku kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa LUPA AMCOS, Chunya.

Mkulima wa chama cha msingi LYESELO(LYESELO AMCOS) Upendo Mwabukusi akiuliza swali kwa kampuni ya ununuaji Tumbaku katika kikao

 cha tathmini ya zao la Tumbaku kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa LUPA AMCOS, Chunya.

Matangazo

  • KUPIGA KURA YA RAIS KITUO AMBACHO HAUKUJIANDIKISHA September 15, 2025
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • DC BATENGA AHIMIZA TIJA KILIMO CHA TUMBAKU KWA VYAMA VYA MSINGI CHUNYA.

    October 17, 2025
  • VIJANA WAIHESHIMISHA CHUNYA KUPITIA MKOPO WA ASILIMIA 10

    October 07, 2025
  • WAKULIMA CHUNYA WANUFAIKA NA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA.

    October 04, 2025
  • UANDAAJI MPANGO WA BAJETI WAWANUFAISHA WATAALAMU CHUNYA DC.

    October 01, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.