• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

AFISA MANUNUZI NA MZABUNI MATATANI

Imewekwa: October 7th, 2019

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amkamate Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka.
Pia alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amkamate na kumhoji Bw. Joseph Kisaka ambaye alikuwa mzabuni wa chuo hicho kwa kuwapatia  vifaa ambavyo ni chini ya kiwango.
Alitoa agizo hilo jana jioni  Oktoba 6, 2019 wakati akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba, mkoani Singida ambako alibaini delivery note ikionesha kitasa kimoja kimenunuliwa kwa sh. 70,000 badala ya sh. 25,000.
Waziri Mkuu alisema quotation ya manunuzi inaonesha kwamba walipaswa kununua vitasa ambavyo vinafunga mara tatu lakini alipokwenda kukagua milango kwenye mabweni, ukumbi, na bwalo alikuta ni vitasa vya kufunga mara moja.
“Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa kila chuo ili kufanya ukarabati wa vyuo vya elimu kikiwemo hiki cha kwenu. Ninyi mnanunua vifaa kinyume na utaratibu wa Serikali, hamvikagui, mnaweka tu vitu hafifu ambavyo havidumu. Haiwezekani!”
“Quotation yenu hapa inanionesha mlinunua vitasa 368 vya 3-level kwa gharama ya shilingi 70,000 kila kimoja. Lakini vitasa vilivyoko mlangoni ni vya 1-level ambavyo vinauzwa shilingi 25,000. Haya ni mabweni ya wanafunzi, wanaingia na kutoka kila wakati, ni kwa nini mnaweka vitu cheap wakati mnajua vitaharibika mapema? Maelekezo ya ununuzi wa Serikali yakoje?”
Alipoulizwa wametumia utaratibu gani kununua vifaa hivyo, Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Hamisi Njau alisema walikuwa wakitumia kamati ya manunuzi ambayo mwenyekiti wake alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo na Katibu wake ni Afisa Manunuzi, Bw. Muyombo.
Bw. Muyombo alipoulizwa kama walikuwa wanayo BOQ ambayo ilikua ikiwaongozwa kufanya manunuzi, alijibu kwamba hawakuwa nayo bali alikuwa wakiorodhesha mahitaji yao na kuyapeleka kwa mhandisi.
Alipoambiwa aeleze tofauti ya vitasa vya 3-level na vya 1-level, Bw. Muyombo alijibu kwamba waliambiwa na mhandisi kwamba ndani ya kitasa kuna kibati ambacho kinatofautisha vitasa hivyo.
Waziri Mkuu alisema Serikali inakataa udanganyifu kwenye manunuzi na haitavumilia watumishi wasiokuwa waaminifu. “Tena hili duka la huyo Kisaka ni la nguo wala siyo la hardware.
Alimwambia Mkuu wa Chuo hicho alipaswa kusimamia ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati unaofanyika chuoni hapo.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitoa sh. 1,439.235,746 ili kukarabati chuo hicho kwenye maeneo ya utawala, maeneo ya kujifunzia, kumbi na mabweni ya wanachuo. Awamu ya kwanza ya fedha hizo iliingia Novemba, 2017 na awamu ya pili ikaingia Juni 2018.
Akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho baada ya kufanya ukaguzi huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini. “Mheshimiwa Rais alitoa sh. bilioni 1.4 kwa vyuo vyote ili kukarabati na kuboresha hadhi ya vyuo hivyo vikiwemo vya Monduli, Patandi, Kinampanda, Mtwara, Songea, Nachingwea, Korogwe, Kasulu na Butimba.”
“Nimeingia kwenye maktaba yenu nimeona bado vitabu vilivyopo ni vya muda mrefu, lakini kwa upande wa ajira bado tunaendelea kuajiri kwa awamu. Julai mwaka huu tuliajiri walimu 4670 na sasa hivi tumepata kibali cha kuajiri walimu 16,000,” alisema.


(mwisho)

IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU

Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • TARAFA YA KIPEMBAWE CHUNYA YAJIDHATITI KUWATUMIKIA WANANCHI.

    March 21, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.